HABARI MSETO (HEADER)


August 20, 2023

ILICHOMKIMBIZA SKUDU HIKI HAPA

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa winga wake Mahlatse Makudubela 'Skudu' ameondoka nchini jana kurudi kwao Afrika Kusini kwa ajili ya kushughulikia zoezi la kupata hati mpya ya kusafiria.

Skudu amepata ruhusa hii ya benchi la ufundi la klabu hiyo kwenda kushughulikia jambo hilo mapema kabla mechi za Kimataifa hazijachanganya na Klabu ikakosa kumtumia.

"Skudu aliumia tulipokuwa Tanga, lakini tayari alishaanza mazoezi mepesi kurejea kwenye timu. Kocha akaona ampe ruhusa muda huu kwenda kushughulikia hati yake ya kusafiria ili kukwepa usumbufu wa safari baadae.

"Hati yake ya kusafiria ya sasa hivi inaelekea kujaa hivyo kumpa nafasi ya kupumzika kupona vizuri amepewa na ruhusa ya kusafiri kulimaliza na jambo hili la hati ya kusafiria haraka," amesema Meneja wa kikosi cha klabu hiyo Walter Harrison.

Skudu anatarajia kurejea nchini tarehe 24 kujiunga na kikosi kuelekea mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya ASAS kutoka Djibout.


No comments:

Post a Comment

Pages