August 30, 2023

MRADI WA UJENZI WA OFISI YA TMA, KANDA YA MASHARIKI NA KITUO CHA KUTOA TAHADHARI ZA TSUNAMI NCHINI WAKAGULIWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi akizungumzia mradi wa ujenzi wa Ofisi ya TMA na kituo cha kutoa tahadhari za Tsunami.


Na Mwandishi Wetu

 

MWENYEKITI Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Kanda ya Mashariki na Kituo cha kutoa tahadhari za TSUNAMI nchini, unaotekelezwa eneo la SIMU 2000 Sinza, Jijini Dar es Salaam.

Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya sh. bilioni tisa, unatarajiwa kukamilika Julai, mwaka 2024.

Akizungumza wakati wa ziara yake, Dk. Nyenzi alisema, chini ya Serikali  inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, TMA  imenufaika na uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ukiwemo mradi huo ambao utahusika na utoaji wa tahadhari za TSUNAMI nchini, hivyo kuongeza tija katika mipango ya nchi.

Dk. Nyenzi alifurahishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea kutokana na hatua mbalimbali ambazo mkandarasi amezichukua ikiwemo kufanya kazi muda wa ziada na kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha makubaliano ya kimkataba yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.

Dk. Nyenzi alisisitiza matumizi ya malighafi zenye ubora na kutoa fursa za ajira kwa wazawa katika mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages