Na Shamimu Nyaki
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) lihakikishe kuwa Mradi wa Baraza hilo ujulikanao kama BASATA
Vibes unawafikia Wasanii mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ili
azma ya Serikali ya kukuza sanaa nchini itimie.
Mhe. Dkt.
Ndumbaro ametoa agizo hilo leo Septamba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam
mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Mradi wa BASATA
Vibes na Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa hapa nchini wenye lengo la
kuimarisha maonesho ya Sanaa, kutoa mafunzo kwa Wadau wa Sanaa na
kuwajengea uwezo wa kuandaa matukio ya burudani.
" Kupitia
Ubalozi wa Ufaransa natumia nafasi hii kwenu Ubalozi kuhakikisha
mashindano ya michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024 uhusishe burudani
kutoka kwa wasanii wetu, hili naomba mlizingatie sana, pia katika
mashindano hayo naomba mhakikishe Watanzania wanapata nafasi za kutosha
kwenye michezo hiyo kwakua vigezo vya kushiriki wanavyo" amesisitiza
Mhe. Ndumbaro.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amesema kuwa atahakikisha jukumu
alilokabidhiwa na Mhe. Waziri la kuwapata Wanamuziki Wazuri na wenye
sifa ya kuburudisha katika mashindano hayo linatimia .
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma akizungumza
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema Sekta hiyo inatoa fursa
kwa Wadau wake kupata nafasi katika soko la Kimataifa.
Aidha,
Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi. Flora Valleur amesema mradi huo pia
utahusisha kujifunza Lugha la Kifaransa, na kupata nafasi kwa wasanii wa
Tanzania kuhudhuria na kutoa burudani kwenye majukwaa ya burudani ya
nchi hiyo
September 17, 2023
Home
Unlabelled
BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI
BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment