Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), yuko Madrid, Hispania, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara, na Utalii wa nchi hiyo, Bi. Xiana Mendez, ambapo Hispania, kupitia Wakala wake wa Bima (Export Credit Agency-ECA), imeonesha nia ya kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kutoa mkopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa kampuni za nchi hiyo zitakazojenga reli hiyo kuanzia Makutopora hadi Mwanza na Kipande cha kuanzia Tabora - Kigoma hadi Malagarasi, kutokana na umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya nchi.
Na Benny Mwaipaja, Madrid, Spain
Hispania
kupitia Wakala wake wa Bima (Export Credit Agency - ECA), imeonesha nia
ya kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kutoa
mikopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa kampuni za nchi hiyo zitakazojenga
reli hiyo kuanzia Makutopora hadi Mwanza na Kipande cha kuanzia Tabora -
Kigoma hadi Malagarasi, kutokana na umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo
ya nchi.
Ahadi
hiyo imetolewa mjini Madrid, Hispania, na Naibu Waziri wa Viwanda,
Biashara, na Utalii, Bi. Xiana Mendez, alipokutana na kufanya mazungumzo
na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambapo pamoja na
mambo mengine, walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi
hizo mbili, ukiwemo ujenzi wa mradi huo mkubwa wa SGR.
Alisema
kuwa Hispania inatambua umuhimu wa mradi huo kwa Tanzania kama ilivyo
kwa nchi hiyo kwa kuwa kukamilika kwake kutaongeza mnyororo wa thamani
wa uwekezaji na biashara na kuwa Kituo cha biashara katika Ukanda wa
Afrika.
Bi.
Mendez alisifu uchumi imara wa Tanzania pamoja na uwepo wa mazingira
mazuri ya uwekezaji, hatua ambayo imezifanya kampuni nyingi kutoka nchi
hiyo kutaka kushiriki katika uwekezaji na ujenzi wa miradi ya
miundombinu itakayochochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo pia
nishati jadidifu.
Aliahidi
pia kuwa nchi yake itafungua Ofisi Dar es Salaam kutokana na kuongezeka
kwa uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya
kurahisisha shughuli hizo za kibiashara.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,
aliishukuru Hispania kupitia Wakala wake wa Bima, kwa kuonesha nia ya
kuziwezesha kampuni za Hispania zitakazofanya shughuli zake za biashara
na ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini Tanzania, ukiwemo Mradi wa
Reli, mikopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa kampuni zinazoshiriki
katika ujenzi wa miradi nje ya nchi hiyo.
“Ushiriki
wa Wakala wa Bima wa Hispania (Export Credit Agency-ECA), katika
kutekeleza mradi huo wa kimkakati ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na kwa
ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu kati ya Hispania na Tanzania, na
kwa maendeleo ya wananchi kwa ujumla” alisema Dkt. Nchemba.
Alisema
kuwa katika kuimarisha uhusiano na maandalizi ya kutekeleza ufadhili
huo wa SGR, Mkandarasi ametafuta kampuni 12 za Kihispania
zitakazosambaza vifaa vitakavyotumika kujenga reli hiyo na kumwomba
Naibu Waziri huyo na Serikali yake kwa ujumla, kuzishawishi kampuni
nyingi zaidi kutoka nchini humo kujitokeza kushiriki katika ujenzi wa
mradi huo.
Mhe.
Dkt. Nchemba alisema kuwa mradi wa SGR ni muhimu kwa Tanzania kutokana
na kuwa lango la biashara kwa nchi 7 za Ukanda wa Afrika na Maziwa Makuu
zisizopakana na Bahari na kwamba utakapokamilika utachochea shughuli za
biashara, usafiri na usafirishaji mizigo na hatimaye kuongeza pato la
Taifa.
Aidha,
Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliishukuru Hispania kwa kufadhili
ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo Mradi wa Umeme Vijijini
(REA), maji, afya, usafirishaji, kilimo, pamoja na Shirika la maendeleo
la nchini hiyo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (FONPRODE), kuonesha nia
ya kutoa fedha kwa ajili ya Mradi wa Uendelezaji Bonde la Mto Msimbazi,
jijini Dar es Salaam.
Zaidi
ya dola za Marekani bilioni 3.24 zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha
ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha tatu, nne na cha tano
kinachoanzia Makutopora hadi Mwanza, na ziara ya Mhe, Dkt Nchemba na
ujumbe wake katika nchi za Ulaya ni kukutana na kufanya majadiliano na
Taasisi za Fedha na wadau mbalimbali, kutafuta fedha za kugharamia
ujenzi wa Reli hiyo.
No comments:
Post a Comment