September 11, 2023

MAFANIKIO YAIPA JEURI NIC INSURANCE KUMWAGA ELIMU KWA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance, Dkt. Elirehema Doriye, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023.




Na John Marwa

NIC Insurance kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya bima itaendelea kutoa elimu ya bima kwa wananchi kupitia vyombo mbalimbali ili watanzania wengi wajiunge na huduma za Bima mfano: Radio, Runinga, Magazeti, Machapisho na  Makongamano.

NIC 'Insurance' ni kampuni inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, ikiwa na dhamana ya kufanya biashara ya bima za mali na ajali pamoja na bima za Maisha.  Kati ya makampuni zaidi ya 30 yaliyopo kwenye soko la bima Tanzania, NIC 'Insurance' imeweza kumudu ushindani huu kwa kufanya vizuri baada ya maboresho mbalimbali yaliyofanyika tangu mwaka 2019.


Hayo yamebainishwa na Dkt. Elirehema J. Doriye Mkurugenzi Mtendaji wa 
NIC Insurance katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

"Kutokana na ukuaji wa NIC katika nyanja mbalimbali ikiwemo mwendelezo mzuri wa kupata faida na ukuaji wa mtaji, NIC  limeendelea kuvutia wateja wa bima kwa vigezo vifuatavyo: Uzoefu, Hekima na Urithi, Thamani, Ubora na Imani, Kuwa na vigezo vya kimataifa vya utoaji wa huduma bora kwa wateja.

"Ongezeko la mitaji Katika kukabiliana na uwezo mdogo wa kuhimili hasara inayoweza kutokea (low underwriting capacity) tumefanikiwa kuongeza mtaji  wa kiasi cha Shilingi bilioni 12.05 mwezi Aprili, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 408.47 kutoka mtaji uliokuwepo wa kiasi cha Shilingi bilioni 2.95 na kufikia mtaji wa kiasi cha Shilingi bilioni 15 kilichopo sasa."amesema na kuongeza kuwa 

"Utoaji wa gawio, Kwa mwaka ulioishia Juni, 2022 tumetoa gawio la Shilingi bilioni 2.0 kwa Serikali ikilinganishwa na gawio la kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 lililotolewa mwaka ulioishia Juni 2021.


"Ukuaji wa Uwekezaji katika hati fungani za Serikali kwa mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Shilingi bilioni 105.64 uKIlinganisha na kiasi cha Shilingi bilioni 51.58 kilichokuwepo mwaka 2019/20. Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 52.40 kwa mwaka. Uwekezaji katika amana za Benki mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Shilingi bilioni 32.23 ukilinganisha na Shilingi bilioni 19.53 kilichokuwepo mwaka 2019/20. Ongezeko hili la uwekezaji kwenye amana za Benki ni sawa na wastani wa asilimia 32.54 kwa mwaka.


" Pia Ukuaji wa mtaji kwa wanahisa Ufanisi katika uendeshaji, umewezesha ukuaji wa Mtaji wa wanahisa kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 72.16 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 217.07 mwaka 2021/22. Ukuaji huu wa mtaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 100.40 kwa mwaka."amesema.

Katika hatua nyingine amesema "Mali za NIC, zimekua kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kutoka mali zenye thamani ya Shilingi bilioni 350.36 mwaka 2019/20 hadi kufikia mali zenye thamani ya Shilingi bilioni 423.99 mwaka  2022. Ukuaji huu ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 10.51 kwa mwaka.


"Faida ghafi imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 33.65 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 63.21 mwaka 2021/22 sawa na asilimia 43.91 kwa mwaka. Aidha, kutokana na faida mfululizo tumeweza kupata malimbikizo ya faida ya Shilingi bilioni 45.74 kufikia Juni, 2022 kutoka kiasi cha malimbikizo ya hasara ya shilingi bilioni 19.31."amesema.

"Tumeweza kulipa kodi ya mapato Serikalini kutokana na faida inayopatinana ambapo ulipaji huo umeongezeka kutoka Shilingi billioni 11.86 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 15.14 mwaka 2021/22 sawa na wastani wa asilimia 13.80 kwa mwaka.

"Katika kipindi cha miaka mitatu tumelipa madai ya bima za wateja ambapo hadi kufikia Juni 2022, tumelipa jumla ya Shilingi bilioni 33.79 kwa bima za Maisha na Shilingi bilioni 40.18 kwa bima za mali na ajali.


"Usimamizi madhubuti wa matumizi pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi kumeongeza ufanisi na kuondoa matumizi yasiyo na tija jambo lililoshusha gharama za uendeshaji na kuongeza faida."amesema na kufafanua kuwa.

"Kutokana na kuchukua hatua nilizozitaja hapo juu tuweza kuondoa hasara kwa kuongeza mapato kutoka Sh. bilioni 76.45 2019/20 hadi Sh. bilioni 103.94 2021/22. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 17.98 kwa mwaka."amesema Dkt. Elirehema.

Mabadiliko ya Utendaji NIC Insurance imekuwa ikitekeleza shughuli zake kwa kuzingatia mwongozo wa uanzishwaji wake (“MEMART”) na Sheria ya Bima Na. 10 ya mwaka 2009.
NIC insurance ilianza kuchukua hatua za mabadiliko ya kiutendaji ili kujiimarisha kibiashara tangu Julai 2019.

No comments:

Post a Comment

Pages