September 17, 2023

Makampuni 5 yasaini Mkataba Uchimbaji Makaa ya Mawe Mchuchuma, yampongeza Rais Dkt. Samia

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Makampuni matano ya Kitanzania yamesaini mkataba wa miaka mitano wa Uchimbaji wa Madini ya Makaa ya Mawe eneo la Mchuchuma Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Akizungumza kwa niaba ya makampuni mengine baada ya kusaini mikataba hiyo Mwekezaji na Mchimbaji wa Madini Ndaisaba George Ruhoro amesema kwa sasa wanaenda kuandika historia na kuongeza ajira na pato la nchi kwa makaa ya mawe waliyokuwa wanayasikia toka wazaliwe sasa wanaenda kuyachimba.


“Kampuni yangu pamoja na makampuni mengine tulikuwa kwenye ushindani mkubwa ila Kwa bahati nzuri kampuni tano ikiwemo na ya kwangu tumefanikiwa kupata mkataba huu hivyo tunaenda kuandika historia yale makaa ya mawe toka tuzaliwe tulikuwa tunayasikia sasa tunaenda kuya chimba na kuongeza ajira Kwa watanzania na kuchangia uchumi Kwa nchi yetu” Amesema Mwekezaji Ruhoro.

Amebainisha kuwa kupitia uchimbaji huo wataongeza pato la nchi kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali hivyo anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaonyesha watanzania mapenzi ya dhati.

“ Rais wetu Mama Samia amesema makaa ya mawe haya yakachimbwe na watanzania na sisi ni mashuhuda wa mapenzi yake ya dhati sasa tunaenda kuyachimba haya makaa ya mawe na kunufaisha taifa letu”Ameongeza Mwekezaji Luhoro.

Ameongeza kuwa wamepewa muda wa miezi sita kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu zote na kuanzia uchimbaji wa makaa ya mawe na kuanzia kuzalisha angalau kwa mwezi mmoja wazalishe tani laki moja na nusu kwani kwa sasa yanahitajika sana Dunia hasa kipindi hiki ambacho Dunia inapambana kupata nishati.

Aidha amesema matarajio yao ni kukuza kampuni zao na kutoa ajira na kuchangia kwenye pato la taifa na kampuni zao kuzidi kukuza na kuchangamkia fursa za uchimbaji wa madini mengine hata nje ya nchi kwani mkataba huo unaenda kuwa mtaji mkubwa kwenye kampuni zao na kukuza ujuzi kwenye uchimbaji.


No comments:

Post a Comment

Pages