Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb), akifuatilia na kusikiliza Mkutano wa Tano wa Tume ya ushirikiano wa kudumu baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Leo Septemba 14, 2023.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb), ameshiriki Mkutano wa Tano wa Tume ya ushirikiano wa kudumu baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023
Mkutano huo ambao umefungwa leo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), huku akiwataka Wananchi kutambua kwamba suala la Ulinzi na Usalama ni la kila mmoja, hivyo watoe ushirikiano kwa Vyombo vya Usalama ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uwepo wa vihatarishi vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), amesema nchi hizi zimekubalina kuimarisha amani na usalama ili ziweze kukuza shughuli za kiuchumi na kuyaletea Mataifa hayo maendeleo.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji Pascoal Ronda, ameeleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji ni wa kudumu na wa muda mrefu hivyo wataendelea kuhakikisha nchi hizo zinakuwa kiuchumi kupitia umoja na amani.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria Mkutano huo wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi ambapo kwa upande wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Kaspar Kaspar Mmuya amehudhuria Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment