Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), akikagua ujenzi wa hosteli katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika chuo hicho, jijini Arusha.
Na. Joseph Mahumi, WF, Arusha
Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameupongeza uongozi wa
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa matumizi na usimamizi nzuri wa fedha
za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo hicho ambayo amesema
imejengwa kwa viwango vinavyolingana na thamani ya fedha iliyotumika.
Mhe.
Chande alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa
miradi inayoendelea katika Chuo hicho ukiwemo ujenzi wa jengo la
Postgraduate na Hosteli, inayotekelezwa kupitia mfumo wa "force
account".
"Hapa
nimeona si thamani ya Fedha tu kwenye hii miradi, bali zaidi ya thamani
ya fedha; nawapongeza sana IAA kwa kazi nzuri mnayofanya, tumeona jengo
lililojengwa kwa bilioni 1.9 ambalo katika maeneo mengine jengo kama
hilo limejengwa kwa gharama kubwa zaidi," alisema Mhe. Chande.
Alisema
kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha inatarajia kutoa jumla ya
shilingi bilioni moja kwa ajili kuendeleza jitahada za ujenzi wa
miundombinu katika Chuo cha Uhasibu Arusha.
Aidha,
katika kuunga mkono jitihada za IAA kwenye uboreshaji wa miundombinu,
Mhe. Chande aliahidi kujenga kisima cha Maji cha kisasa ili kuendelea
kuboresha upatikanaji wa huduma ya Maji.
Kwa
upande wake Naibu Mkuu wa Chuo hicho anayesimamia Mipango, Fedha na
Utawala, Dkt. Cairo Mwaitete, aliishukuru Serikali kwa kuendelea
kuiwezesha IAA kutekeleza mipango yake na kuendelea kutoa huduma kwa
wananchi.
Aliongeza
kuwa Fedha zote zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi
mbalimbali pamoja na zinazopatikana kwa mapato ya ndani zitasimamiwa
vema na zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta tija na matokeo
chanya.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Felician Mtahengerwa, alisema kuwa Chuo
cha Uhasibu Arusha, kimekuwa mfano bora na wa kuigwa kwenye matumizi ya
mfumo wa "force account" katika ujenzi wa miradi hususani kwenye
matumizi na usimamizi mzuri wa fedha, ukamilishaji wa miradi kwa wakati
na thamani ya fedha kwenye miradi husika.
No comments:
Post a Comment