September 27, 2023

MSD YAIMARISHA UPATIKANAJI WA DAWA

Na John Marwa


BOHARI ya Dawa (MSD) imeimarisha upatikanaji wa Bidhaa za Afya kwa mwaka 2022/2023 ambapo juni 2022 ulikuwa asilimia 51 na kupanda hadi asilimia 64 Juni 2013, wakati upatikanaji wa Dawa umefika asilimia 81 mwezi juni 2023 kutoka asilimia 57 juni 2022.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Upatikanaji wa bidhaa za afya umeongezeka kutoka asilimia 51 mwezi juni 2022 hadi kufikia asilimia 64 juni 2023. Wakati upatikanaji wa Dawa umefikia asilimia 81 mwezi juni 2023 kutoka asilimia 57 juni 2022.

“Ongezeko la fedha kwa ununuzi wa bidhaa za afya, fedha iliyopokelewa mwaka wa fedha 2022/23 ni Tsh bilioni 190.3 ikilinganishwa na Tsh bilioni 134.9 mwaka wa fedha 2021/22 sawa na asilimia 95.


“Utekelezaji wa mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa vifaa vya huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua (CEmONC), awamu za utekelezaji ni tano, idadi ya vituo vya kutolea huduma vinavyopelekewa huduma ni 284. Huku jumla ya vifaa vilivyosamabzwa hadi kufikia juni 2023 ni 299 sawa na asilimia 87.” Amesema Tukai na kuongeza kuwa.


“Gharama za Mradi, Thamani ya vifaa vinavyotarajia kusambazwa Tsh bilioni 99.7, thamani ya vilivyosambazwa ni Tsh bilioni 79.4. Asilimia za uekelezaji ni asilimia 80.

Utekelezaji wa mradi wa Uviko-19 unahusu hospitali na vituo vya vingine vya kutolea huduma za afya. Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo MSD imetekeleza ni kama zifuatazo; Kigoma, Kagera, Lindi, Katavi na Lugalo.


“Gharama za mradi huo, thamani ya vifaa vilivyotarajiwa kusambazwa ni Tsh bilioni 17.17 huku thamani ya vifaa vilivyosambazwa ni Tsh bilioni 17.62 sawa na asilimia 102 za utekelezaji.” Amesema Tukai.


Wakati huo huo MSD imefanikiwa kwenye ununuzi wa vifaa vya afya kwa kuanzisha kitengo cha Maalumu cha Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mikataba.


“Ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka shil bilioni 14.1 mwaka wa fedha 2021/22hadi kufikia shil bilioni 39.77. kutoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, zile ambazo zinakidhi mahitaji na viwango vya ubora hivyo kutegemea wazalishaji wa ndani.

“Kuanzisha zabuni malumu zinazohusu wazalishaji wa ndani hivyo kuongeza uwezo wa uzalishaji. Kuongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka 2022/23.” Amesema Tukai.  


USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA AFYA


“Kuimarisha mfumo wa usambazaji kwa kusambaza bidhaa za afya mara 6 kwa mwaka (kila baada ya miezi miwili) kwa mwaka wa fedha 2022/23 badala ya mara nne kwa mwaka (miezi mitatu) hivyo kupunguza muda wa vituo vya afya kusubiri bidhaa za afya.


“Kununua matrela 16 yenye thamani ya Sh, bilioni 2.6 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za afya, kuongeza usambazaji wa bidhaa za afya kwa asilimia 16 kutoka Sh, bilioni 320 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi Sh, bilioni 373 kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Kutumia mifumo ya shirikishi ya TEHAMA (PoD) ili kuhakikisha bidhaa za afya zinapokelewa kielekitroniki katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuimarisha ufuatiliaji wa magari kwa kutumia mifumo.” Amesema Tukai.


MAFANIKIO YA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA AFYA

“Kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha mipira ya mikono “gloves” kilichopo Idofi, Njombe. Kuhusisha sekta binafsi kwa kutambua maeneo ya uwekezaji wa bidhaa za afya za kimkakati za vidogo (tablets), rangi mbili (capusules), vimiminika na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza matamanio ya ushirikiano kati ya MSD na Sekta binafsi.


Kukamilisha taratibu za usajili na uendeshaji za kiwanda cha barakoa cha N95 kilichopo Keko ambapo uzalishaji wake utakidhi mahitaji ya barakoa nchini.



Uanzishaji wa Kampuni tanzu “MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd” itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya.” Amesema Tukai.

No comments:

Post a Comment

Pages