September 07, 2023

SOKO LA BIDHAAA KUTOA ELIMU KUWAFIKIA WADAU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania, Godfrey Malekano, akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo wakati wa mkutano na Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Septemba 7, 2023, ukiwa ni mwendelezo wa mikutano ya taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Hazina kutoa taarifa za utendaji kazi kwa kipindi cha miaka mitano. Na Mpiga Picha Wetu.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Manyerere Jackton akitoa neno la shukrani wakati wa mkutano uliowakutanisha Wahariri na Waandishi wa Habari na Soko la Bidhaa Tanzania juu ya utendaji kazi wa taasisi hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na
Ofisi ya Msajili wa Hazina.


 

Na John Marwa


Soko la Bidhaa litaendelea kutoa elimu na kuwafikia wadau wengi zaidi ili wafahamu mchango wake katika uchumi wa nchi, hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania, Godfrey Malekano alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Amesema Soko la Bidhaa litaendelea kujiendesha kwa ufanisi, kidijitali na kutoa huduma zake kwa uadilifu ili kulinda maslahi ya washiriki wake wote

"Kazi ya kujenga mfumo imara wa Soko la Bidhaa inategemea mchango wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi hivyo basi ushirikiano ni muhimu sana kufikia adhima hiyo.

"Soko la Bidhaa litaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na wadau husika ili kuongeza bidhaa zaidi Soko la Bidhaa litaendelea kushirikiana na wanahabari kwani kupitia wao ni rahisi kuufikia umma wa Watanzania." Amesema Malekano na kuongeza kuwa.

"Dira na dhima ya Soko la Bidhaa Ni Kuwa Soko linaloongoza, anuwai zaidi na linalokwenda na wakati katika nchi za Afrika mashariki, kati na kusini.

"Kutoa huduma za kisasa, zenye ufanisi kwa uwazi na uadilifu kupitia jukwaa la kuaminika la mauzo ya bidhaa kwa njia ya teknolojia ya hali ya juu katika kutekeleza na kutimiza malengo ya maendeleo ya Taifa." amesema.

Maana ya Soko la Bidhaa, Soko la Bidhaa Tanzania ni mfumo rasmi unaokutanisha wauzaji na wanunuzi kwa pamoja na kufanya biashara ya mikataba ya bidhaa, inayotoa uhakika wa ubora, ujazo na malipo.

"Soko hili huleta wanunuzi wengi wa ndani na nje ya nchi ambao sio lazima wafike kwenye soko la bidhaa au nchini kwa kuwa mauzo katika Soko la Bidhaa hufanyika kwa kutumia Mfumo wa Kidijitali ambao huwawezesha wanunuzi wa bidhaa kufanya manunuzi popote walipo ndani na nje ya nchi." amesema.

Amebainisha kuwa Mfumo wa Kielektroniki unaendelea kuboreshwa kuongeza bidhaa zaidi kwa ajili ya mauzo.

"Mfumo wa Kielektroniki wa TMX unaweza kuhusisha “Reverse auctions” ambapo wanunuzi wanaweza kutangaza kununua kiasi fulani cha bidhaa ya daraja maalum katika eneo maalum la kuwasilisha, na wauzaji kushindana kwa bei kwenye mfumo wakati wa mauzo (trade sessions).

"Kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa TMX vinatokana na bei za Soko la Kimataifa kama vile Nasdaq Futures na London International Financial Futures Exchange (LIFFE) na maendeleo ya mahitaji na ugavi ya ndani ya nchi.

"Mabango ya Kidijitali (Electronic Display Units) yanaendelea kuwekwa katika baadhi ya maeneo ya kimkakati kwa ajili ya usambazaji wa taarifa za bei na soko kwa wadau na umma." Amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages