HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 08, 2023

TTCL YAWEZESHA INTANETI YA KASI KONGAMANO LA CONNECT 2 CONNECT (C2C) ZANZIBAR


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

 

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) ikiwa ni kitovu cha mawasiliano imefanikisha huduma ya intaneti ya kiwango cha juu inapatikana kwa wajumbe wanaoshiriki Kongamano la Connect 2 Connect (C2C) la Kimataifa linalofanyika Jijini Zanzibar ili kuwawezesha kuperuzi kwa uharaka na urahisi masuala anuai.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw. Vedastus Mwita amesema huduma hiyo ya intaneti imefanikiwa kutokana na uwepo wa Miundombinu imara inayotolewa na shirika hilo.


 "TTCL si tu kama mtoa huduma za mawasiliano ya simu bali kama mhusika mkuu aliyepewa mamlaka ya kupanga, kujenga, kuendesha na kudumisha miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano ya simu, ambayo inaweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya kisasa ya kiteknolojia na miundombinu hiyo pia imeundwa ili kuendana na mwingiliano wa waendeshaji ndani na nje ya Tanzania," alisema Bw. Mwita.

Aidha amesema kwa sasa TTCL imefanya mabadiliko makubwa katika Kuboresha utoaji wa huduma ambapo imehakikisha miundombinu ya mawasiliano ya simu kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) umeboreshwa zaidi ambapo kwa sasa unapakana ndani ya nchi 8 zikiwemo Kenya, Congo, Rwanda, Burundi, Malawi na Uganda.


 Hata hivyo, Bw. Mwita aliongeza kuwa pamojja na hayo, TTCL pia inahakikisha shughuli nzima ya uhifadhi wa data inafanikiswa kwa kutoa suluhisho na vifaa vya kutunza Data kupitia Kituo cha kutunza Data Kimtandao (NIDC) kilichoidhinishwa na ISO kinafanya shughuli hizo kiufanisi zaidi.

Sambamba na hilo amebainisha TTCL inahakikisha inakuwa ndio Lango la huduma za E-Serikali kwa kukaribisha miundombinu na huduma muhimu za ICT, Lango la usalama wa kitaifa wa kielektroniki kwa kuimarisha usalama wa sekta ya mawasiliano.

Kongamano hilo la siku mbili lililofanyika kuanzia Septemba 6 hadi 7, 2023 katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr visiwani Zanzibar limewakutanisha wadau zaidi ya 250 wa TEHAMA na lengo likiwa ni kushirikishana masuala mazima ya Ukuaji wa Teknolojia, fursa mbalimbali za Kibiashara pamoja na Ushirikano wa Kibiashara.


No comments:

Post a Comment

Pages