Jumla ya wahitimu 554 wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametunukiwa shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa Mahafali ya 22 ya chuo hicho.
Mahafali hayo yalifanyika Disemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) ambapo Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein alisema kuwa kuna haja ya kuendeleza maeneo ya ardhi ya Chuo ambayo yapo jijini Dar es Salaam kwa kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo na zenye mwelekeo wa baadae.
Dkt. Shein amesema Chuo hicho kikiwa na ukumbi mzuri wa aina yake itakuwa ni jambo la maana na fahari kwa chuo na jamii inayowazunguka, na kuongeza kuwa wanaweza kujenga ukumbi wao unaokidhi haja na mazingira ya kisasa
kwa kutumia shughuli zao rasmi na kukodisha watu wengine ili kujiongezea
kipato.
Licha ya hayo ameoumba uongozi wa Chuo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya kusomea katika eneo la Kituo cha Tegeta Ndaki ya Dar es Salaam ambako wanafunzi ngazi ya Shahada ya Kwanza wanasoma pia kutokana na uwingi wao watakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo.
Dkt. Shein ameeleza kuwa kutokana na kuwa na ndaki tatu sasa wanakamilisha ndaki ya Tanga ambayo itakamilika muda mchache ujao ili kuendelea kutoa elimu kwa maendeleo ya watu kama. Kauli mbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe inavyosema.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, William Mwegoha amesema kuwa kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kilisajili jumla ya wanafunzi 1,699 Ndaki ya Dar es Salaam.
Baadhi ya hao, ndiyo watakaohitimu katika mahafali hayo.
Katika mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam jumla ya wanachuo 554 wamehitimu katika ngazi mbalimbali za kitaaluma na kustahili kutunukiwa shahada mbalimbali.
Katika ya hao, wahitimu 428 wametunukiwa Shahada za Umahiri na wahitimu 126 wamenukiwa Shahada ya Awali.
Kwa mwaka wa masomo 2022/23, idadi ya wahitimu wa Wanawake ni 311 sawa na asilimia 55.30 na wanaume ni 243 sawa na asilimia 44.70.
“Ni jambo la kujivunia na furaha sana kuona uwiano mzuri kati ya wahitimu wanawake na wanaume. Sisi kama Chuo Kikuu Mzumbe tutaendelea kupanua fursa na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuhakikisha kuwa uwiano huu unadumishwa mwaka hadi mwaka.” Amesema Prof. Mwegoha
Pia amewapongezawaitimu wote kwa kuhitimu masomo yao na amewaomba wakatumikie jamii na taifa kwa ujumla wakatumie vizuri maarifa, elimu na stadi walizopata Chuo hapo
“Elimu na stadi mlizopata kutoka Chuo Kikuu Mzumbe viwe chachu ya kuleta maendeleo chanya katika jamii inayowazunguka, taifa na dunia kwa ujumla.
Pia amewaomba wakawe mabalozi wazuri wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwa waadilifu na wachapakazi bora.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwatunuku Shahada wahitimu katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Disemba 14, 2023.
No comments:
Post a Comment