HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2023

Benchika aipigia hesabu kali Kagera Sugar

Na John Marwa

WAKATI Simba inashuka dimbani leo dhidi ya Kagera Sugar, Uongozi wa timu hiyo umekana kuhusishwa na usajili wa nyota watatu, Lameck Lawi wa Coastal Union na Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar pamoja na Eric Mbangossoum kutoka Union Touarga Sportif ya Morocco 

Umesema ni mapema kuzungumzia usajili huo kwa sababu  benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Abdallah Benchikha linafanya tathimini juu ya nani wa kumuingiza katika eneo lipi na nani wa kutoka Simba.



Tayari Simba inahusishwa kumalizana na nyota wawili, mmoja ni mzawa ambaye ni Chasambi na Eric wanaotajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watajiunga na kikosi cha wekundu hao katika usajili ya dirisha dogo lililofunguliwa hapo kesho desemba 16.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema zoezi lote la usajili liko mikononi mwa kocha Benchikha ambaye amefanya tathimini ya kikosi chake na kuona wapi na nani anaweza kuongeza nguvu.

“Kwa sasa ni mapema sana kuzungumza lolote juu ya usajili na nani anaingia au kutoka, hilo ni jukumu la kocha ambaye amefanya tathimini ya timu yake na tunatarajia kupata mapendekezo juu ya nafasi na wachezaji wataongezwa kikosini.

Muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi kwa sasa akili na nguvu zetu kuelekea mechi zilizopo mbele yetu, tunakibarua kigumu cha kutafuta pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar baada ya hapo kuna Wydad Casablanca kuwapeleka moto hapa nyumbani na kuacha alama ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” Amesema Ahmed.

Kuelekea mchezo wao dhidi Kagera Sugar unaotarajia kucheza leo saa 10:00 alasiri, uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kocha Benchikha amesema baada ya safari ndefu kutoka Morocco wamerejea na kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kuvuna alama tatu katika mchezo huo aa ligi kuu.


Amesema amepata fursa ya kuona taarifa za wapinzani wao na ameaandaa kukosi chake kwa ajili ya ushindani mkubwa kulingana na ubora wa mchezo huo.


“Tunahitaji ushundi, tunawaheshimu wapinzani wetu , kwa upande wangu hii mechi ni muhimu sana baada ya hapa nitaifikiria Wydad Casablanca. Hakuna mechi rahisi na kila mchezo umekuwa na maandalizi yake.


Kuwepo kwa mfululizo wa mecho kila baada ya siku mbili au tatu hilo haitakuwa na athari kikubwa ni kuandaa timu kulingana na mpinzani unayekwenda kucheza naye,” alisema Benchikha.


Mwakilishi wa wachezaji kwa upande wa Simba, Ally Salim amesema wamejiandaa vizuri kwenda kuwakabili wapinzani wao Kagera Sugar kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages