HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2024

BARRICK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA WA MASHINE YA PATIENT MONITOR HOSPITALI YA RUFAA MWANANYAMALA

Afisa Mawasiliano wa Barrick, Neema Ndossi (kulia) akikabidhi msaada wa mashine ya Patient Monitor, kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,Dkt. Zavery Benella.Wengine pichani ni Wafanyakazi wa Barrick alioongozana nao.


Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, na kukabidhi msaada wa mashine ya kudhibiti maendeleo ya kiafya ya watoto waliozaliwa na matatizo (Neonatal Patient Monitor).

Akiongea wakati wa kukabidhi kifaa hicho kwa uongozi wa hospitali hiyo, Afisa Mawasiliano wa Barrick, Neema Ndossi, aliyeambatana na baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wakiungwa mkono na wafanyakazi wenzao Wanaume alisema “Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake, mwaka huu tumeona tutoe fadhila ya msaada wa Patient Monitor kwa ajili ya kusaidia watoto wachanga wanaozaliwa na matatizo katika hospitali hii.”

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Zavery Benella, ameishukuru Barrick na wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa katika wodi ya watoto.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,Dkt. Zavery Benella, akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick waliotembelea hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dkt. Zavery Benella (kushoto) akitoa maelezo ya huduma za hospitali hiyo kwa wafanyakazi wa Barrick walipotembelea wodi ya watoto.
Mwonekano wa mashine ya Patient Monitor iliyokabidhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Wafanyakazi wa Barrick katika picha ya pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Dkt. Zavery Benella.

No comments:

Post a Comment

Pages