HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2024

Senyemule awataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria

Na Jasmine shamwepu, Dodoma

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyemule amewawataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria ili kuepusha ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.


Akizungumza na wadau sekta ya Usafirishaji na usalama barabarani amewataka wasimamizi wa ujenzi kuzingatia viwango katika ujenzi ili kulinda usalama wa watumiaji.



Aidha ameongeza kuwa mafunzo haya ya mda mfupi yatawezesha Wahandisi,wasanifu wa barabara,wasimamizi wa Sheria wadau wa usalama barabarani na wachunguzi kwa ajili ya barabara kupata maarifa ya kuzingatia katika Ukaguzi wa barabara.



Katika hatua nyingine Senyemule amesema lengo la kuchunguza usalama barabarani na vyanzo vya ajali zinazotokea wakati wa matumizi ya barabara na kuongeza tija katika vituo vya kazi kwa Maafisa wa usalama barabarani.



Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha usafirishaji NIT Dkt. Zainabu Mshana amesema kuwa katika kufikia Malengo ya mradi wa EASTRIP na kuleta tija kwa Taifa chuo kilijiwekea Malengo matano ikiwemo lengo la kuzifikia taasisi zingine ambazo zipo nje ya mradi na kutoa mafunzo kama haya.



"Hadi sasa Washiriki Wapatao 908 wamepata ufadhili na kulipwa ada za mafunzo ya mda mfupi kupitia fedha za mradi huo katika Nyanja za usafirishaji kutoka kanda mbalimbali nchini"Amesema Dkt. Mshana.



Hata hivyo baadhi ya wananchi wakizungumza na BLOG  hii wameziomba mamlaka husika na matengenezo ya barabara kuimarisha kitengo Cha ukaguzi wa barabarani na kuzifanyia marekebisho Kwa wakati sehemu zenye uharibifu hasa katika kipindi hiki Cha masika kwani barabara nyingi zimeharibika jambo ambalo si salama Kwa wasafiri na watumiaji wa barabara hizo.


No comments:

Post a Comment

Pages