March 02, 2024

CCM KIBAHA MJI YAMPIGA JEKI YA MAGONGO KIJANA ALIYEVUNJIKA MGUU KWA AJALI

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA


Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini Issack Kalleiya ametimiza ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa msaada wa magongo  kwa kijana mmoja anayeishi katika kata ya Msangani.

Kijana huyo ambaye anajulikana kwa jina la John William amepatiwa msaada huo baada ya kupata ajali ya kupushiwa na Lori hivi karibuni na kupelekea mguu wake wa kulia kuvunjika kwa chini.

Katibu huyo wa CCM alike da kutoa msaada huo akiwa ameambatana na viongozi mbali mbali wa chama sambamba na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mji Mwalimu Mwajuma Nyamka pamoja na baadhi ya wananchi wengine.

Katibu huyo alisema kwamba alipokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa hiyo ya kijana wa CCM kupata ajali hivyo aliahidi kwenda kumuona pamoja na kumpatia msaada huo wa magongo.

"Kwa kweli mimi kama kiongozi niliguswa sana na tukio hili la kijana wetu wa ccm ambaye kwa kweli nikaona kuna umuhimu kumsaidi kwa hali na mali magongo ambayo yataweza kumsaidia katika kufanya mazoezi ya kutembea,"alifafanua Katibu huyo.

Kadhalika alisema kwamba  kijana
huyo amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na vijana wenzake kwa lengo la kukilinda na kukiimarisha chama katika mambo mbali mbali.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji Mwalimu Mwajuma Nyamka naye  alifika nyumbani kwa kijana huyo kwa ajili ya kumona na kumfariji.

Naye Kijana huyo John William aliyepata ajali alimshukuru kwa dhati Katibu wa CCM kwa moyo wake wa upendo wa kumpatia magongo hayo na kuwashukuru viongozi wote wa CCM waliokwenda kumjulia hali na kumpa pole.

No comments:

Post a Comment

Pages