March 02, 2024

Katibu Mkuu wa CCM ashiriki kuaga mwili wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan, Jumamosi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama   Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole mmoja wa Wajane wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Bi Siti Mwinyi (aliyekaa), baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, shughuli iliyofanyika Jumamosi, Machi 2, 2024, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akimpatia pole Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi (Mb), ambaye ni mmoja wa watoto wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi,  baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

Pages