RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendeleza utaratibu wake wa futari ya pamoja na wananchi mbalimbali.
Futari
hiyo maalum aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye
ukumbi wa Sheikh Iddriss Abdul Wakiil, Kikwajuni Wilaya ya Mjini, ikiwa
ni mwendelezo wa utaratibu uliojiwekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kila ifikapo mwenzi Mtukufu wa Ramadhani kufutarisha wananchi na
waumini wa dini ya Kiislam wa visiwa vya Unguja na Pemba.
Utaratibu huu hujenga umoja, ushirikiano, mshikamo, upendo pamoja na kuimarisha amani baina ya viongozi na wananchi.
Al
hajj Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo, kuwashukuru wananchi hao kwa
kuitikia wito wa kujumuika pamoja naye na kuusifu uongozi wa Mkoa huo
kwa kufanikiwa kugusa makundi yote ya jamii zenye uhitaji.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Iddris Kitwana Mustafa, akizungumza kwenye
hafla hiyo, amemshukuru Rais Al hajj Dk. Mwinyi kwaniaba ya wananchi wa
Mkoa huo kwa kujumuika pamoja nao kwenye futari hiyo.
Miongoni
mwa wananchi waliojumuika kwenye futarisho hilo ni pamoja na wazee,
wajane, watu wenye ulemavu, watoto, watoto yatima, na wananchi wenye
uhitaji.
Aidha, hafla hiyo ya futari ya pamoja pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment