HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 25, 2024

Dk. MWINYI afutarisha Mjini Magharibi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendeleza utaratibu wake wa futari ya pamoja na wananchi mbalimbali.


Futari hiyo maalum aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye ukumbi wa Sheikh Iddriss Abdul Wakiil, Kikwajuni Wilaya ya Mjini, ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu uliojiwekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kila ifikapo mwenzi Mtukufu wa Ramadhani kufutarisha wananchi na waumini wa dini ya Kiislam wa visiwa vya Unguja na Pemba.

Utaratibu huu hujenga umoja, ushirikiano, mshikamo, upendo pamoja na kuimarisha amani baina ya viongozi na wananchi.

Al hajj Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo, kuwashukuru wananchi hao kwa kuitikia wito wa kujumuika pamoja naye na kuusifu uongozi wa Mkoa huo kwa kufanikiwa kugusa makundi yote ya jamii zenye uhitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Iddris Kitwana Mustafa, akizungumza kwenye hafla hiyo, amemshukuru Rais Al hajj Dk. Mwinyi kwaniaba ya wananchi wa Mkoa huo kwa kujumuika pamoja nao kwenye  futari hiyo.

Miongoni  mwa wananchi waliojumuika kwenye futarisho hilo ni pamoja na wazee, wajane, watu wenye ulemavu, watoto, watoto yatima, na wananchi wenye uhitaji. 

Aidha, hafla hiyo ya futari ya pamoja pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa.


No comments:

Post a Comment

Pages