Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuacha mizozo isiyokuwa na tija inayopelekea kuleta mifarakano baina yao na kukosa maelewano katika jamii jambo lilalomchukiza Allah (S.W).
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid INTISWAM uliopo KIZIMKAZI Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema kuwa suala la kuwepo mizozo na ugomvi katika jamii zetu hupelekea kukosekana kwa maendeleo na kukosa neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa mshikamano na maelewano kwa wananchi ndio chanzo cha maendeleo ya katika Taifa lolote lile hivyo amewataka waumini kuwa na utamaduni wa kusameheana wanapokoseana kama alivyoamrisha Allah (S.W) na kusisisirizwa na Kiongozi wa Umma wa Kiislam Mtume Muhammad (S.A.W).
Alhajj Hemed amesema waumini ni lazima kuwa wamoja wenye Kupendana, kushikamana na kuwa wavumilivu baina yao ili kuweza kuwarithisha vizazi vyao kuweza na kuwataka kuitumia misikiti kama ni sehemu ya mazungumzo yanayojenga jamii iliyoimara.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewasisitiza wazazi na walezi kuwawekea mazingira mazuri vijana wao kwa Kuwapatia Elimu zote mbili ya Dunia na Ya Akhera ili kuweza kupata warithi ambao wataitetea nchi yao na dini kwa ujumla.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim SAID RAMADHAN amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kujitahidi kufanya ibada kwa wingi za faradhi na Sunna, kusoma sana Qur-an na kutoa sadaka kwa mwenye uwezo ili kupata Maghafira kutoka kwa Allah (S.W)
Amesema kuwa ni lazima kwa waumini wa dini ya kiislamu kuhakikisha wanakesha katika kufanya ibada hasa kwa masiku haya yaliyobakia katika mwezi mtukufu wa ramadhani huku wakitarajia kupata fadhila kutoka wa mwenyezi mungu (S.W) kwa kila jambo hasa kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhan
No comments:
Post a Comment