HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 29, 2024

ASKARI WAWILI WAJERUHIWA AJALI YA MOTO MLANDIZI

Na Mwandishi Wetu, Pwani 

 

ASKARI wawili  wa Jeshi la  Zimamoto   na uokoaji  wamejeruhiwa  wakiwa katika  harakati za  kuokoa  marehemu  waliokuwa  wamenasia  kwenye gari baada ya kuzuka moto ghafla na magari kuwaka moto.



Hayo yamesemwa leo Machi 28  na Kamanda  wa Polisi Mkoa  Mkoa wa Pwani  (SACP) Pius Lutumo alipozungumza na  Waandishiwa Habari.

RPC Lutumo amewataja askari waliojeruhiwa kuwa ni Koplo Elias Bwire na Koplo Hamisi Kungwi wote wamekimbizwa Hospitali ya Taifa  Mloganzila kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

" Machi 28  mwaka huu majira ya  saa 10:15 alfajiri  katika bonde la Ruvu  Wilaya  ya  Kipolisi Mlandizi,  Mkoa wa Pwani  barabara   ya Morogoro, Dar es Salaam  gari namba T668 DTF aina ya Scania  Kampuni  ya  Sauli ikiendeshwa na dereva  Idd Aloyce (35),mkazi wa  Mafinga  ikitokea Dar es Salaam  kwenda Mbeya liligonga ubavuni  lori  la mafuta ya Petroli  lenye namba za usajiri RAF672N na tela  lenye namban RL2594 aina  ya Howo  lililokuwa  linatoka Dar es Salaam kwenda nchini Rwanda likiendeshwa  na dereva  Mushimana Musiyimana lililokuwa limesimama kupisha gari lililokuwa linakuja mbele yake".



 Aidha  basi hilo lilikuwa  limeongozana  na basi la Golden Deer Kampuni ya New Force lenye namba za usajiri RAF672N na likiendeshwa na dereva aitwaye Burton Jacob (33),.mkazi wa Mbeya  ambapo nalo lililigonga kwa nyuma basi la Saul lililokuwa mbele yake na kusababisha vifo vya watu wawili ambao hawakufahamika majina yao na majeruhi watatu ambao ni Salimu Daud (50) mkazi wa Mbozi  Mbeya, Farida Idrisa (26)mkazi wa Tabata Dar es Salaam  na Kiambile Geofrey  mkazi wa Uyole Mbeya.

RPC Lutumo chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva wa mabasi yote mawili kushindwa kuchukua tahadhari kwa kuyapita magari mengine lakini pia kushindwa  kutunza umbali  kati ya gari moja   na lingine huku yakiwa yamefatana.

"Pamoja na hayo uchunguzi wa awali unaonesha   kuwa chanzo  cha moto huo  ni hitilafu ya injini ya basi la Saul iliyokua imekita chini baada ya kugonga  gari lingine  na kuripua petroli wakati wa uokoaji"amesema RPC Lutumo.

"Wito  wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Pwani unawataka madereva  kutii sheria  za Usalama Barabarani  kwa mujibu wa taaluma zao na ifahamike kwamba madereva  wanachukua dhamana  kubwa ya maisha na mali za watu"

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema atayafungia mabasi yatakayoendelea kuvunja  Sheria za Usalama Barabarani baada ya ajali iliyotokea alfajiri ya leo.

RC Kunenge  amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kibaha Mkoani Pwani, amesema yeye ameamua kwa kushirikiana na wanaotoa lesseni, LATRA na Jeshi  la  Polisi  kuwa wataweka mkakati wa kudhibiti ajali ndani ya Mkoa wa Pwani.


"Mtagundua kuwa  Mkoa wa Pwani hii Barabara ni kubwa na mabasi yakitoka kule stendi kuu ya Dar es salaam Mbezi idadi ya  mabasi  ni mengi yakiwa yamekaguliwa lakini bado hapa pia tunakagua " amesema.



No comments:

Post a Comment

Pages