March 16, 2024

MAKARANI WA USIMAMIZI WA UCHAGUZI WA UDIWANI MSANGANI WAFUNDWA

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

 

Katika kuelekea katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Udiwani kata ya Msangani iliyopo Halmashauri ya mji Kibaha makarani wa kusimamia uchaguzi huo wamepatiwa mafunzo maalumu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Uchaguzi huo wa kujaza nafasi ya udiwani wa kujaza  nafasi hiyo unnatarajiwa kifanyika machi 20 mwaka huu ambapo utawashirikisha wananchi wa kata ya Msangani.

Kadhalika  Makarani hao  waongozaji licha ya kupata  mafunzo hayo wamepata  kiapo cha kutunza Siri Chini ya Kanuni ya 16(1) (a) na 50 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni ya 14 (1)(a),(2) na 43(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani),2020 Mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Salum Papen.

Aidha,Mafunzo hayo yametolewa na Maria Israel,Benjamin Mputtu wakisaidiana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Optuna Kasanda ambao wamewasisitiza kwenda kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi

Akifungua Mafunzo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi,Mwanasheria nguli wa Mahakama kuu na zilizo chini yake Salum Papen amesema.." Tume imewateua ninyi kwa mujibu wa sheria na Kwa kuzingatia uzoefu wenu katika masuala ya Uchaguzi "katendeni haki amesisitiza Papen

Papen ametoa rai kwa Makarani waongozaji kujiamini na kujitambua,kufanyakazi kwa kuzingatia Katiba ya Nchi,Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake,Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbambali yanayotolewa na Time

Katika hatua nyingine Makarani wametia tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa na Chama cha Siasa chini ya Kanuni ya 16 (1)(b) na ( 3 ) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni 14(1) (b) na (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,(Uchaguzi wa Madiwani),2020 mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi,Mwanasheria Salum Papen

Aidha,Andrea Isamaki Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) ameshiriki kushuhudia Mafunzo,kiapo cha kutunza Siri na tamko la kujitoa uanachama kwa Makarani waongozaji

Nadia Issa na Benson Shawa,Makarani waongozaji wamesema wanakwenda kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi

Uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya udiwani katika Kata ya Msangani unatarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu  kutokana na kifo cha Mhe.Leonard Mlowe kilichotokea tarehe 23 Disemba,2023 ambapo jumla ya vyama nane (8) vya Siasa vinatarajia kushiriki.



No comments:

Post a Comment

Pages