March 16, 2024

SERIKALI IMEWATAKA WAKURUGENZI NA WATENDAJI WA MASHIRIKA YA MASLAHI YA WACHACHE KUSIMMIA MASLAHI YA UMMA

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga mkutano kati ya Msajili wa Hazina na Wakurugenzi wa bodi ya maslahi ya wachache uliofanyika Kibaha Mko wa Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida wakifuatilia kwa makini hotuba ya Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, aliyoitoa wakati wa kufunga mkutano wa  kati ya Msajili wa Hazina na Wakurugenzi wa bodi ya maslahi ya wachache uliofanyika Kibaha Mko wa Pwani. 





 

Na Mwandishi Wetu

 

Serikali imewataka wakurugenzi na wajumbe wa bodi katika taasisi na makampuni ambayo Serikali ina hisa chache kwa maslahi ya wachache kusimamia maslahi ya umma katika taasisi wanazozisimmia kwa niaba ya Serikali na Taifa kwa ujumla.

 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo wakati akifunga Mkutano wa siku tatu kati ya Msajili wa Hazina na Wakurugenzi wa bodi ya maslahi ya wachache, uliofanyika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.

“Mhe Rais anamini na ana Imani kwamba na taasisi za umma na makampuni ambayo serikali ina uwekezaji, yana nanafsi kubwa sana ya kuchangia katika maendeleo ya nchi hii na kwa sababu hiyo ameamua kuweka mkono kwenye kufanya mabadiliko katika taasisi hizo ili zifanye kazi na ufanisi wake uweze kuonekana.” Amesema Kitila.

Amesema yapo mabadiliko mbalimbali yanafanyika kisheria na kiuteandaji ili kuhakikisha taasisi hizo zinaendelea kuzalisha kwa faida ya uchumi wa nchi na maendeleo ya taifa.

“Mabdiliko mengine ambayo yanahitajika ni mabadiliko ya kimtazamo kwamba hizi taasisi za umma ili ziweze kuwa na mafanikio lazima ziendeshwe kama kampuni za kibishara sasa hapo yanahitajika mabadiliko ya kimtazamo, zijitazame hivyo, zijione hivyo na zienende hivyo.

Mna nafasi nzuri ya kutupatia uzoefu ni kwa nini shirika ambalo linamilikiwa na serikali kwa asilimia mia halifanyia vizuri lakini likibinafsishwa kwa asilimia kadhaa linafanya vizuri, tupeni uzoefu wa mashirika binafsi namna gani yanafanikiwa ili tasisi za serikali tuweze kuzisaidia.” Amesema Kitila na kuwapongeza washiriki wa mkutano huo.

“Niwapongeze nyie wote kwa mafanikio ambayo taasisi zenu zimeyapata katika shughuli ambazo mnazifanya na tunaamini mafanikio ya taasisi hizo yanachangiwa na uzoefu wenu mkubwa katika kuwa sehemu ya juu ya kuzishauri na maamuzi ya taasisi hizo.

Lakini pia amewashauri kutumia muda wao kujifunza kupitia wawekezaji wan je katika makampuni na taasisi walizopo ili uzoefu huo wautumie kuishauri serikali namna gani ya kuendesha taasisi na mashirika yake.

Awali alimshukuru Msajili wa hazina kwa kumualika kwenda kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika Chuo cha Mwalimu Nyerere Mkoani Pwani.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema Mkutano huo umewasaidia watu kuweza kujuana na kujifunza mambo mapya lakini pia kuweza kuondoka na ajenda moja ya nini amabacho serikali inahitaji wao kuweza kufanya na kusimamia katika taasisi na makampuni wanayoyasimamia.

 

 “Dhima yetu kubwa ilikuwa ni ‘Uzalendo wa kiuchumi katika Uwekezaji wa Umma’. Lakini pia tumetoka na maazimio matano ambayo tutayazungumza kwako ili yaweze kueleweka.

“Sisi kama Ofisi ya Msajili tutahakikisha kunakuwa namafunzo ambayo yataongeza ujuzi na uwajibikaji kwa wakurugenzi na wasimamizi, tukihizimiza pia taasisi na makampuni kuhakikisha nao wanafanya hivyo”amesema Mchechu.

No comments:

Post a Comment

Pages