Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO,ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema kuwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni hifadhi ya tatu kwa ukubwa nchini yenye Kilomita za mraba 14,763.
"Hifadhi kubwa zaidi nchini ni Nyerere yenye ukubwa wa Kilomita za mraba 30,893 ikifuatiwa na hifadhi ya Ruaha yenye Kilomita za mraba 19,822 lakini Serengeti ndiyo hifadhi ya kwanza nchini kwa kuingiza watalii wengi zaidi.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dodoma leo Machi 10, Matinyi amesema kuwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo za hifadhi bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo, Serengeti ni maarufu zaidi kwa tukio la uhamaji wa wanyama aina ya Nyumbu (Immigration),ambapo kila mwaka nyumbu wapatao Mil.1.5 hutumia miezi kumi wakizunguka ndani ya hifadhi ya Serengeti na kisha kwenda nchi jirani na kurudi,katika uhamaji huo tukio la kusisomua zaidi ambalo ndilo huvutia watalii wengi ni like la kuvuka Mto Mara pamoja na matawi yake.
"Kufuatia mafanikio ya filamu ya Royal Tour ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alikua ameshiriki mkuu jambo linalowavutia watalii,idadi ya watalii wanaokuja Serengeti imeongezeka kupita malengo makubwa yaliyowekwa kwa mwaka huu wa fedha.
Matinyi amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Utalii Duniani (World Travel and Tourism Council -WTTC),kwenye ripoti ya Tanzania ya Februari 2023 inaonesha asilimia 90.7 ya wageni wanaoingia nchini hutembelea vivutio vya hifadhi za Taifa ya Ngorongoro na fukwe za Zanzibar.
"Rekodi zinaonesha kuwa kati ya Julai 2023 hadi Februari 2024 watalii kutoka nje ya Afrika Mashariki ni 10,531,watalii wa Afrika Mashariki ikiwamo Watanzania ni 230,785 wafanyakazi wa hotel kambi na madereva ni 46,702.
"Hifadhi za Taifa 21 zilizo chini ya TANAPA zina barabara zenye urefu wa jumla ya Kilomita 16,470.6 ambapo Serengeti peke yake ina jumla ya Kilomita 3,176"amesema Matinyi.
Amesema kuwa hifadhi ya Serengeti ndiyo yenye mtandao mrefu zaidi wa barabara ambazo ni za udongo ama changarawe,barabara hizi zimegawanyika katika barabara kuu zilizo chini ya Wakala wa barabara Tanzania (TABROAD) na wakala wa barabara za Vijijini TARURA na kundi la pili la barabara ndogondogo zilizo chini ya TANAPA yenyewe.
Aidha Matinyi amesema kuwq katika mtandao Kilomita 3,176 za barabara za Hifadhi ya Taifa Serengeti KM.2,407 niza udongo na KM7.69 ni za changarawe ,kutokana na hoja kadha wa kadha za kiuhifadhi hakuna barabara za lami wala zege.
"Ilipotokea changamoto ya mvua za El Nino kulitokea mafuriko makubwa hifadhini kiasi cha kufunika barabara kuu zinazotumika kuleta watalii ,uharibifu ulikua mkubwa hivyo basi TANAPA ilichukua hatua za haraka za awali za kuzifanyia mayengenezo barabara hizo ili kuhakikisha kwamba wageni wanaendelea kutalii na usafirishaji haukwami".
"Hatua za kati TANAPA inataka kunyanyua barabara nzima ya Golini,Naabi hadi Seronera KM.68 kwa wastani wa sentimenta 50 (nusumita) kutokana na ukaguzi uliofanyika ili kuifanya iwe juu kidogo ya usawa wa ardhi hivyo kuruhusu maji kutoka barabarani yapite kwenye mifumo ya mifereji na mitaro ya maji iliyopo pembezoni mwa barabara na kazi hii inaendelea.
No comments:
Post a Comment