March 20, 2024

Miaka 3 ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Tanzani yang'ara Kidiplomasia Mara dufu


Na Magrethy Katengu--Jamuhuri Media Dar es Salaam

Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi  Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani Tanzania imepata Mafanikio makubwa ikiwemo kung'ara Kidiplomasia  Duniani kote.


Akizungumza leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Januri Makamba amesema katika kipindi  cha miaka mitatu ishara inayoonyesha kuwa Tanzania imeng'ara Kidiplomasia namna  takwimu zinavyoonyesha kiwango cha Uwekezaji mtaji 2020 ilikuwa dola bilion 1.03 uliongia huku mwaka 2023 mtaji uliongia kutoka kwa wawekezaji ni bilion 5.6.

Makamba amesema kuwa Jambo ambalo nchi inatafuta kuongeza ni  Ushawiahi Duniani ili ipate misaada, mikopo ,wawekezaji waje ambapo miaka mitatu ya Uongozi wa Rais   idadi kubwa ya wageni, mahitaji ya sauti yake , kauli yake kutafutwa katika mambo muhimu nje ya nchi akitolea  mfano Rais alipokuwa Zanzibar kuna Vingozi wakubwa walitoka nje ya nchi kumfuata awashauri hii inaonyesha namna gani Rais Dkt Samia Suluhu Hassani anavyokubalika na busara zake zinavyohitajika.

"Nchi yetu imekuwa ikipata maendeleo na kutekeleza miradi yake ya kimkakati kwa kupata mikopo ya mashariti nafuu pia misaada hiii inachagizwa na ushawishi mzuri ukiongonzwa na Mwanadiplomasia mzuri Rais wetu ambapo pia kupitia yeye wageni wamekuwa wakija kutembele  Tanzania huku mialiko mingi ikija  hii  haitokei kama kiongozi hana Ushawishi sisi sote tujivunie kuwa na Rais mwenye upekee wa aina yake " amesema  Waziri


Katika hatua nyingine WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba amezindua kamati maalum itakayosimamia na kushughulikia chuo Cha uhusiano wa kimataifa Diplomasia cha Salim Ahmed Salim.

Makamba amesema wajumbe wa kamati walioteuliwa wanasifa na wabobezi katika nyanja ya diplomasia za kimataifa na pia wameitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali nchin

Aidha kamati hiyo yenye wajumbe saba huku mwenyekiti wake wao akiwa ni Balozi Khamis Kagasheki na makamo wake akiwa ni balozi Ramadhani Dau.wengine ni Profesa Masilina Chinoriga (mjumbe), Dk Salim Ali (mjumbe), Dk Singo (mjumbe), Ashumta Muna (mjumbe), Dk Shule (mjumbe), Dk Sanga (mjumbe)

Kazi za kamati: Makamba amezitaja kazi za kamati hiyo kuwa ni pamoja na kupendekeza muundo wa kisheria wa uongozi wa kituo aina ya mafunzo na mitaala ya chuo, Kamati inatakiwa kuwa na uwezo wa kubuni fikra za aina ya uongozi wa chuo, Kupendekeza muundo wa uombaji wa ajira kwa watu mishi na wafanyakazi wa chuo pia itakuwa na kazi ya kujua ni namna Gani chuo kitaweza kuiendesha ikiweno kubuni namna ya njia za kujipatia pesa za kujiendesha chenyewe pia imepewa kazi ya kutoa maoni na ushauri kwa wizara kwa jambo lolote ambalo litakuwa na tija kwa chuo.

Waziri  Makamba amekumbusha kuwa chuo cha uhusiano wa diplomasia cha salim Ahmed Salim ni moja ya chuo kikongwe barajni Afrika kilichojizolea sifa nyingi kutokana na kuzalisha viongozi wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Naye mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Khamis kagasheki kwa upande wake amemshukuru mheshimiwa Waziri Makamba na kamati yake kwa uteuzi wake na Imani kubwa waliyonayo kwake.

Aidha balozi kagasheki ameitaka kamati hiyo kufanyakazi kwa nguvu moyo, ueledi,kijituma Uzalendo kwa Taifa kwani wao ni kati ya watanzania wengi waliopata bahati ya kuitumikia kamati  hiyo

No comments:

Post a Comment

Pages