March 16, 2024

Serikali kuandaa mpango wa dira mpya ya Taifa kwa kushirikiana na wadau

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa mashirika  ya umma iliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani.
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Amon Nnko, akizungumza wakati akitoa maadhimio ya mkutano huo.

Baadhi ya washiriki.

 


Picha ya pamoja.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akiagana na washiriki wa mkutano huo.

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Serikali ya awamu ya sita imepanga kuandaa mpango wa dira mpya ya Taifa kwa kushirikiana na wadau ambao utaweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

Waziri Mkumbo ameyabainisha hayo wakati wa kufunga rasmi semina ya siku tatu iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa mashirika  ya umma ambayo yamejadili mada kumi ambazo zitasaidia kuleta maendeleo.

Mkumbo alibainisha kwamba ana imani mpango huo wa dira ya Taifa utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa kushirikiana na sekta binafsi.

"Kitu kikubwa kama serikali kwa sasa tunajipanga kwa ajilli ya kuandaa dira mpya ya Taifa kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali ili kuweza kuwa na mpango wenye kuleta tija katika siku zijazo "alisema Professa Mkumbo.

Kadhalika amebainisha kwamba kwa sasa ajenda kuwa ya nchi ni kuhakikisha inaongeza thamani katika mazao ili yaweze kuwa na ubora na kuuzika katika nchi za nje.

Alibainisha kuwa serikali ikiweka mkazo mzuri katika suala zima la kuongeza thamani ya mazao kutaweza kusaidia zaidi katika kukuza uchumi wa nchi.

Aidha aliwataka watendaji kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta ushindani zaidi na makampuni ya kutoka  nchi  nyingine za nje .

Mkumbo pia alibainisha kuwa serikali kwa sasa ina ajenda nyingine kubwa ya kuona madini ya kimkakati yaliyopo nayo yanaongezewa thamani ili kuyatumia na yaweze kukuza pato la Taifa.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu alisema kwamba mkutano huo umeweza kuwakutanisha mashirika ya umma na kufungua fursa za kupanga mipango ambayo itasaidia nchi kupata maendeleo.

Mchechu alibainisha kwamba katika mkutano huo wameweza kujadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na serikali katika kukuza kasi ya uchumi na maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Amon Nnko amesema wamepitisha maazimio matano katika mkutano huo ambayo yatasaidia katika kukuza uchumi.

Kadhalika aliongeza kuwa katika maazimio hayo ni kuweza kupambana na mwenendo wa hali ya uchumi duniani kufanya mafunzo ya awali,pamoja na kulinda maslahi.

Mkutano huo ambao umefanyika kwa siku tatu katika shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha Pwani umewashirikisha baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma na kuudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na taasisi binafsi.

No comments:

Post a Comment

Pages