March 29, 2024

TRC yajivunia kufikia kiwango cha juu kukamilisha Mradi wa SGR miaka mitatu ya Rais Samia



 Na Hussein ndubikile, dar es salaam


Shirika la Reli nchini (TRC) limebainisha Ujenzi wa Miundombinu ya Reli unaotarajia kufikia takribani Trillion 23.3 ikiwa  shilingi trilioni 10 zimeshalipwa kutekeleza Mradi huo wa kimkakati ili kuhakikisha watanzania wanaanza kutumia reli ya SGR mapema.

 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirika hilo,Masanja Kadogosa alipokuwa akizungumza Katika Mkutano wa wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo vya ambapo amesema  zaidi ya Asilimia 70 ya Bajeti ya serikali imewekezwa katika ujenzi wa  Reli ya Umeme (SGR) ambapo ujenzi huo  itapunguza kero ya mizigo Bandarini.


Kadogosa amesema  Wajerumani walikuwa na wazo la kujenga Reli ya (SGR)miaka mingi iliyopita lakini leo hii Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza  kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki.


Amebainisha kuwa  Ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar hadi Makutopola tayari umeshafikia Asilimia 97 ambapo kwa Mwaka fedha 2024/25 wanatarajia kuanza  Ujenzi wa SGR katika Mikoa ya Tanga ,Moshi na Arusha.


Hata hivyo Shirika la Reli (TRC), limepokea maombi kutoka kampuni za uendeshaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika uendeshaji wa reli.


Amefafanua kuwa Serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017, ikiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utoaji huduma za usafirishaji kupitia miundombinu ya reli, hatua inayolenga kuchochea ushindani, ufanisi na ubunifu katika sekta hiyo.


Ameongeza kuwa jitihada za serikali katika kuwekeza sekta ya reli zimejikita kuboresha miundombinu ya reli iliyopo, ujenzi wa reli mpya ya kiwango cha Standard Gauge, na ununuzi wa vitendea kazi kama injini na mabehewa.

"Tunategemea Machi mwaka huu kupokea vichwa vya treni vilivyochongoka jitihada hiyo.inatokana na fedha zilizotolewa kusaidia mradi wa SGR uanze kazi mara moja iwezekanavyo ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi" amebainisha Kadogosa

Kadogosa amesema pia tayari seriki imeshaingia mkataba na Benki ya Dunia wa ujenzi wa Reli ya (SGR ) Tabora hadi Isiaka huku Mradi wa Dar es salaam hadi Makutupora tayari ukiwa umefik asilimia 97 na Majaribio ya Treni ya Umeme ikiwa imefanya ziara yake ya majaribio


Aidha katika hatua nyingine TRC imezindua Jarida linaloelezea Matukio Miaka Mitatu ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan toleo namba 35 Januari hadi Desema 2023 hivyo haliuzwi anayehitaji kusoma linapatikana mtandaoni na ofisini TRC


No comments:

Post a Comment

Pages