Na Hussein ndubikile, dar es salaam
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirika hilo,Masanja Kadogosa alipokuwa akizungumza Katika Mkutano wa wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo vya ambapo amesema zaidi ya Asilimia 70 ya Bajeti ya serikali imewekezwa katika ujenzi wa Reli ya Umeme (SGR) ambapo ujenzi huo itapunguza kero ya mizigo Bandarini.
Kadogosa amesema Wajerumani walikuwa na wazo la kujenga Reli ya (SGR)miaka mingi iliyopita lakini leo hii Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki.
Amebainisha
kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar hadi Makutopola tayari
umeshafikia Asilimia 97 ambapo kwa Mwaka fedha 2024/25 wanatarajia
kuanza Ujenzi wa SGR katika Mikoa ya Tanga ,Moshi na Arusha.
Hata
hivyo Shirika la Reli (TRC), limepokea maombi kutoka kampuni za
uendeshaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, ambao wameonesha
nia ya kuwekeza katika uendeshaji wa reli.
Amefafanua
kuwa Serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka
2017, ikiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utoaji huduma za
usafirishaji kupitia miundombinu ya reli, hatua inayolenga kuchochea
ushindani, ufanisi na ubunifu katika sekta hiyo.
Ameongeza
kuwa jitihada za serikali katika kuwekeza sekta ya reli zimejikita
kuboresha miundombinu ya reli iliyopo, ujenzi wa reli mpya ya kiwango
cha Standard Gauge, na ununuzi wa vitendea kazi kama injini na mabehewa.
"Tunategemea
Machi mwaka huu kupokea vichwa vya treni vilivyochongoka jitihada
hiyo.inatokana na fedha zilizotolewa kusaidia mradi wa SGR uanze kazi
mara moja iwezekanavyo ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi" amebainisha
Kadogosa
Kadogosa
amesema pia tayari seriki imeshaingia mkataba na Benki ya Dunia wa
ujenzi wa Reli ya (SGR ) Tabora hadi Isiaka huku Mradi wa Dar es salaam
hadi Makutupora tayari ukiwa umefik asilimia 97 na Majaribio ya Treni ya
Umeme ikiwa imefanya ziara yake ya majaribio
Aidha
katika hatua nyingine TRC imezindua Jarida linaloelezea Matukio Miaka
Mitatu ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan toleo namba 35
Januari hadi Desema 2023 hivyo haliuzwi anayehitaji kusoma linapatikana
mtandaoni na ofisini TRC
No comments:
Post a Comment