HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 27, 2024

Wafanyakazi CRDB watoa ‘Mkono wa Pasaka’ kwa Watoto Yatima Green Pastures

Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo (katikati), Meneja wa Kanda ya Pwani, Badru Idd (wa pili kulia) na Meneja wa CRDB Tawi la Mbagala, Albert Michael wakikabidhi kwa pamoja zawadi ya mbuzi kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Green Pastures Home, Douglaus Mcharo Kiseu (kushoto) na Mama Mchungaji Naomi Kameta (wa kushoto).


Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB.



Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Green Pastures Home, Douglaus Mcharo Kiseu, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka Benki ya CRDB.


Mwenyekiti wa Mameneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani,
ambaye pia ni Meneja wa Benki ya  CRDB Tawi la Mbagala, Albert Michael, akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Green Pastures Home kilichopo Mapinga wilayani Bagamoyo.

 

Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo, akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha kulelea Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Green Pastures Home kilichopo Mapinga wilayani Bagamoyo.


Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bunju, Christina Makwi, akizungumza katika hafla hiyo.







Picha ya pamoja.


Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika hicho.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika hicho.
Mwakilishi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho akitoa neno la shukrani.

Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo akiwa na watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Badru Idd, akiwa na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Msafara wa magari ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB ukielekea katika Kituo cha Green Pastures cha Mapinga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka kwa Watoto Yatima na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu wanaotunzwa kituoni hapo.


 

 

NA MWANDISHI WETU

 

 WAFANYAKAZI wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, kupitia michango yao binafsi, wamekabidhi misaada mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka kwa Watoto Yatima na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu wanaotunzwa na Kituo cha Green Pastures cha Bunju, jijini Dar es Salaam.

Hafla ya makabidhiano hayo iliyoenda sambamba na wafanyakazi hao kuwafungulia Watoto wote akaunti za CRDB, imefanyika kituoni hapo leo Jumatano Machi 27, ambako wafanyakazi hao wakiongozwa na Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo, walikabidhi mchele, mafuta ya kupikia, mbuzi wa nyama, sabuni na bidhaa nyinginezo.

Akikabidhi msaada huo, Lugambo aliwapongeza Mchungaji Douglas Mcharo Kiseu na mkewe kwa moyo wa majitoleo ya kukusanya na kuwaweka pamoja Watoto yatima na wanaoishi kwenye mzingira magumu na kuwatunza kwa upendo kana kwamba wa kuwazaa.

“Tunakupongeza Mchungaji na mama kwa hiki ambacho mnakifanya, zamani hali haikuwepo, lakini siku hizi yapo, yani mtu unamzaa mtoto wako mwenyewe lakini ni shida tupu, hata kama haujamtelekeza, bado uko naye lakini ni shida tupu wewe na wanao hamuelewani.

“Lakini nyinyi kukusanya na kukumbatia Watoto ambao hamjawazaa, tena waliotokea kwenye mazingira na changamoto mbalimbali, mkaishi nao vema, Mungu awazidishie, awaongezee uwezo na awazidishie upendo na wao waje kuwa wazazi wema siku za usoni,” alisemaLugambo

Naye Meneja wa CRDB Tawi la Mbagala, Albert Michael, ambaye ni Mwenyekiti wa Mameneja wa Matawi ya CRDB Kanda ya Pwani, alisema wafanyakazi wa Kanda yake wamekuwa na utaratibu wa kuchangisha fedha kutoka katika mishahara yao na vyanzo vyao vingine vya mapato, kisha kununua mahitaji ya kijamii.

Kisha, mahitaji hayo kuyakabidhi kwa vituo mbalimbali vyenye uhitaji, hasa katika nyakati za mfungo wa Kwaresma kwa Wakristo na Mfungo wa Ramadhani kwa Waislamu.

“Lengo la kufanya hivi ni kuwasaidia yatima na wenye uhitaji, ili Kwenda sambamba na tafakari na kumbukumbu juu ya mwenyezi Mungu, kuwawezesha nao kujua kwamba wana thamani na hawajasahaulika na kwamba sisi tupo kwa ajili yao.

“Tumechanga kidogo kidogo kwa kila mfanyakazi wa Kanda ya Pwani, na kilichopatikana kikatumika kufanya manunuzi ya mahitaji haya ili tuweze kuwasaidia wenzetu wenye uhitaji wajue kuwa wanakumbukwa.

“Tumefanya hivyo ili kutoa sadaka kwa ajili yao, huku tukiamini kuwa hata watoto wetu wanaweza kuwa katika vituo hivi na kuhitaji kisha kusaidiwa na watu wasiowafahamu.

“Kwa hiyo leo tumekuja hapa Green Pastures kukabidhi msaada huu, tutafanya hivyo pia kwa vituo vingine viwili kabla ya Sikukuu za Pasaka na Idd, kituo kimoja kiko Tandika hapa jijini Dar es Salaam na kingine kiko Zanzibar.

Akitoa neno la shukrani kwa msaada huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Green Pastures, Mchungaji Douglas Mcharo Kiseu, aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kuwakumbuka na kuwapelekea msaada huo, ambao umekuja kwa wakati muafaka, huku akiomba taasisi zingine kujitokeza kusaidia.



“Hilij ambo kwakweli limetubariki sana mahali hapa, nitoe rai kwa taasisi zingine na wadau kwa ujumla, ziguswe na hali ngumu zilizopo katika vituo vya yatima na kujitoa kusaidia, watutembelee au watembelee vituo vingine kama hiki, kwani shida ni nyingi sana.

“Watakapofabnya hivyo, basi kwa pamoja tutakuwa tunajenga jamii iliyo na afya na nguvu na mwisho wa siku Mungu atatubariki sote,” alisema Mchungaji Kiseu na kuongeza kuwa:

“Hapa kwetu Green Pastures tuna changamoto kubwa ya bima za afya kwa Watoto. Bima kwa sasa zimekuwa changamoto kubwa na hapa kwetu hatuna bima kabisa na tunaishi kwa kumuomba Mung utu.

“Kituo chetu kina Watoto 37 na wote hao hawana bima hata mmoja, tunaiomba Serikali, Taasisi za Fedha na Wadau wa maendeleo, kutusaidia kwa hili, sio hapa Green Pastures tu, bali katika vituo vingi kuna aina hii ya changamoto zinazohitaji utatuzi,” alimaliza Mchungaji Kiseu.


No comments:

Post a Comment

Pages