March 21, 2024

ZARI HASSAN "BOSS LADY"AONGEZEWA MKATABA WA UBALOZI NA KAMPUNI SOFTCARE

Na Magrethy Katengu-- Dar es Salaam

 

 Zari Hassan kwa jina maarufu (Boss lady )ambaye ni mzazi mwenza wa msanii, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amewaomba wadau na mtu mmoja mmoja kuwasaidia wanafunzi wakike wanaoshindwa kumudu gharama za kununua taulo za kike.



Akizungumza leo Machi 21,2024 katika hafla yake fupi  kuongeza mkataba wa kutangaza bidhaa za kampuni ya Softcare, amesema amesema anashukuru sana Kampuni hiyo kumwamini tena hivyo hapo kesho anakwenda hospitali ya Taifa Mhimbili kutoa sadaka yake kwa kutoa pempasi kwa watoto wadogo na baadhi ya wakina mama taulo za kile kwani kutoa ni moyo si utajiri .

"Ninamchukuru sana Mungu wa Mbinguni kwa kunipa kibali tena kuongezewa mkataba na Kampuni hii kutangaza bidhaa zake ambazo ni za uhakika na ubora mimi nimekuwa nikizitumia pia watoto wangu wakiwa wadogo hivyo niwahakikishie kuzitumia.

Pia katika Mahojiano yake amesema yeye ni Mzazi na amempa sifa msanii Zuhura Othman ‘Zuchu’ kwamba ni mlezi mzuri wa familia na ana tabia nzuriwatoto wake wakija Tanzania wanapata malezi kutoka kwa Zuchu ambaye ni mwenza wa Diamond kwa sasa, hivyo binafsi anakuwa na amani sana kwamba wapo katika mikono sahihi na wanafurahi kuwa naye na wanampenda.

Zari raia wa Uganda anayeishi Afrika Kusini, ametoa kauli hiyo leo katika mkutano na wana habari baada ya kuulizwa swali kama anajisikiaje watoto wake wakija Tanzania wanavyolelewa na mwanamke mwingine.

No comments:

Post a Comment

Pages