April 13, 2024

AKILI ZA KUSHIKIWA NI AKILI MFU KWENYE KICHWA CHA ALIYEHAI

Na John Richard Marwa 


Kelele zimekuwa nyingi sana huko Msimbazi, kila mmoja na kilio chake, vilio ambavyo havijaanza leo.


Najaribu kuwaza kwa sauti kuhusu Simba na maisha yao, Simba na mashabiki wake na mashabiki na Simba yao.

Wakati wengine wakiruka majivu na kukanyaga moto kuna  wanaoruka mkojo na kukanyaga kinyesi.

Niwaulize wana Simba, ni kweli timu yenu ni mbovu kutokana na wachezaji mlionao ama ni mbovu kwa sababu ya kelele za walala hoi wanaotafuta njia ya kwenda msalani isiote nyasi??

Ni kweli mmechoka na hamuoni wachezaji wenu wanaipambania timu kwa Nguvu zao zote kama ambavyo wamekuwa wakifanya toka mlipojipata??

Ni kweli Mangungu ndio tatizo na Try Again na kama ndio kwanini mlimrudisha kwenye kiti kwa niaba yenu afu mnalia??!

Ni kweli Muhene ndio tatizo kutoka kwa Mwekezaji? Mbona hamkuhoji kwenye mkutano Mkuu au matumbo yenu yana Nguvu zaidi ya akili zenu.

Ni kweli mnalogwa ama timu yenu inalogwa au kuna vitu haviko sawa ama Ile miaka minne mliloga mkawa bora sana na mganga mmemsahau ???

Ni kweli Mo ndio tatizo? Hatoi hela? Ameiacha timu ? Kumbe mnaweza kumlipa Benchika, Miquisone, Chama, Saido kwa kelele zenu za kwenye magroup ya WhatsApp na Instagram???

Mo hatoi hela na nyie mmeshika corous mnaimba hata mishipa ya aibu hamna, Mmemleta nyie Ngoma, Ayoub, Fondoh na Sarry??

Kwani Ile bajeti mliosomewa imeenda wapi hadi leo mlie Mo hatoi hela?

Ni kweli mnamiliki asilimia 51 za Simba na Mo anamiliki 49 afu mnamlilia Mo ama hizo 51 ni hewa dhidi ya 49 ambazo zinatoka kwa Billionea Mo??

Msiniulize hizo 51 mnazichangiaje kwa sababu nitawauliza 49 zinawapaje furaha ikiwa hamna pa kuiweka.

Mnapenda sana kusikia ya kuambiwa kuliko mnayoyaona, mna macho hamuoni, masikio yamechagua kusikia yanayowaumiza afu mnalia na mnamtafuta anayewaliza?!! .

Msiposhutika mtazikwa mkiwa hai hii ni Afrika, aliimba FID Q.

Matatizo yenu ni nyie wenyewe, Simba mmechagua matatizo ila hamuyapendi🤔.

NB. Mtalia kila aina ya vilio kama msipouheshimu mpira wa miguu kuanzia viongozi na nyie mashabiki kwani hakuna wa kuwafuta machozi.

Kumbukeni walio waambia timu yenu ni mbovu, hamna wachezaji wa maana mara oooh wachezaji wenu wazee mara Mangungu ndio tatizo,  mara mtimueni Chama amekuwa Mkubwa kuliko timu ndio haohao wanaowaambia MO DEWJI HATOI HELA maana yake hata wao hawajui shida yenu ila mnaamini wanayowaambia!!!!

Usiamini maneno ya kuambiwa kuliko mnayoyaona na kuyaishi.

No comments:

Post a Comment

Pages