April 13, 2024

Wajishindia mamilioni baada ya kufungua NMB PESA AKAUNTI


Kaimu wa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Mwalimu Mbwambo, akizungumza wakati wa kuendesha Droo ya mwezi kwa wateja wa Benki hiyo ambapo jumla ya wateja watano walijinyakulia zawaidi ya Sh.milioni 1 kila mmoja,kulia kwake ni meneja mauzo wa Benki hiyo kanda ya Kusini Roman Degeleki.

Meneja Mauzo wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Roman Degeleki (kulia), akikabidhi zawadi ya kofia mteja wa benki hiyo tawi la Songea mkoani Ruvuma, Emily Lucas mkazi wa Paradiso baada ya kufungua akaunti mpya inayofahamika kwa jina la PESA AKAUNTI wakati wa kucheza Droo ya  kila mwezi ambapo wateja watano walijinyakulia zawaidi ya Sh.milioni 1 kila mmoja

 

Na Mwandishi Wetu

 

Wateja watano wa Benki ya NMB wamejinyakulia  fedha taslimu shilingi milioni moja kila mmoja katika Droo ya kila Mwezi iliyochezwa katika tawi la NMB Songea  kupitia kampeni kubwa inayofahamika kwa jina la Pesa Akaunti.

 

Wateja walioshinda Droo hiyo ya mwezi ni Alhami Shemkay ,Msimu Mwnyimvua, Abdala Msimu, Emanue Masawe ,na unior Mtweve.

 

Pesa akaunti ni Droo maalum inayoendeshwa na Benki hiyo ikihamasisha Watanzania kutumia Benki ya NMB kuweka fedha,kufungua akaunti,na kupata mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo.

 

Meneja wa mauzo wa NMB Kanda ya kusini Roman Degeleki amesema,akaunti ya Pesa Akaunti inafunguliwa kwa gharama ndogo kuanzia Sh.1,000 na haina kianzio cha fedha na mteja hapewi kadi badala yake anaunganishwa moja kwa moja na simu yake ya mkononi.

 

Amesema,akaunti hiyo inamwezesha mteja kufanya matumizi na malipo mbalimbali ikiwemo kulipa Luku,kununua King’amuzi,kulipa bili za maji na vitu vingine kulingana na mahitaji ya mteja husika.

 

Kulingana na Meneja huyo,kupitia Pesa akaunti mteja  anaweza kuchukua mkopo hadi Shilingi laki tano kupitia simu yake ya mkononi bila kuweka dhamana yoyote na kurejesha mkopo huo kwa kutumia simu yake.

 

Degeleki ametaja,faida nyingine ya Pesa akaunti kuwa ni  mteja kupata Bima ya simu ambayo ikipata changamoto yoyote Benki ina uwezo wa kuifanyia matengenezo simu hiyo bila kujali gharama zake.

 

Ametoa rai kwa Watanzania,kuchangamkia fursa hiyo kwa kuendelea kufungua akaunti na kuweka fedha kwenye Benki ya NMB ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa katika kila Wilaya na Mkoa hapa nchini.

Kaimu meneja wa NMB Tawi la Songea Mwalimu Mbwambo amesema,Droo ya mwezi imewahusisha  wateja ambao waliweka fedha kwenye akaunti zao kuanzia kiwango cha fedha kisichopungua Sh.50,000.

 

Kwa upande wake Mkaguzi na Mdhibiti wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Salim Bugufi amesema,kampeni hiyo inafanyika chini ya uangalizi wa Bodi hiyo ili kujiridhisha mtu anayepata fedha hizo kuwa ni mteja halali ya NMB.

 

Mkazi wa kijiji cha Ligera wilayani Namtumbo Silaji Mango,ameipongeza Benki hiyo kwa kuendesha Droo hiyo ambayo imehamasisha watu wengi kutumia Benki ya NMB kwa kufungua akaunti na kuweka fedha.

.


 

No comments:

Post a Comment

Pages