April 05, 2024

BENKI YA CRDB YAWAGUSA WATOTO YATIMA TANDIKA

Mtoto Faisal Athuman (kushoto) akipokea zawadi ya Mbuzi kwa niaba ya watoto wenzake wa Kituo cha Zimamussalikin cha Tandika Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa Benki ya CRDB walipofika katika kituo hicho kutoa sadaka ya vitu mbalimbali. 


Mlezi wa Kituo hicho, Sarah Abdallah akipokea zawadi ya keki.

Baadhi ya watoto wanaotunzwa katika kituo hicho.


 

Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB.

Msafara ukiwasili kituoni hapo.

Meneja wa Tawi la Tandika.


 
Mwenyekiti wa Matawi ya Benki ya CRDB, Albert Michael, akizungumza wakati wa hafla ya kutoa sadaka kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha  Zimamussalikin Tandika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Zimamussalikin kilichopo Tandika jijini Dar es Salaam, Adam Matembelela, akizungmza  wakati wa hafla ya kupokea sadaka kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya watoto wa kituo hicho.


 Diwani wa Tandika, Uzairu Athuman akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kupokea sadaka kutoka benki ya CRDB kwa ajili ya Kituo cha Yatima cha Zimamussalikin.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Pwani, Badru Idd, akitoa hotuba yake wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipofika kutoa sadaka katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Zimamussalikin kilichopo Tandika jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa sadaka katika kituo cha watoto yatima cha Zimamussalikin  kilichopo Tandika jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd (kulia), akiagana na Diwani wa Kata ya Tandika, Uzairu Abdul Athuman, wakati wafanyakazi wa benki ya CRDB walipofika katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Zimamussalikin cha Tandika jijini Dar es Salaam kutoa sadaka kwa ajili ya watoto hao.





 

 


Na Mwandishi Wetu

 

BENKI ya CRDB imetoa misaada ya vitu mbaimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha Zimamusalikin kilichopo Tandika, Temeke jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika tukio la kutoa Mgeni Rasmi Meneja wa CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd ameahidi kuendelea kushirikiana na kituo hicho ikiwemo kutatua cghangamoto zilizopo kituoni hapa ikiwani sehemu ya kumsaidia na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuwatumikia watanzania.


“CRDB imekuwa mstari wa mbele kwelikweli, kama mnaweza kusoma kwenye vyombo vya habari mtaona tunavyoendelea kushirikiana na  jamii hii hii ambako sisi ndiko tunakotoka tufanyeje kazi nayo kwa ukaribu ili kuweza kuwafariji.
Kwa kuwa katika kituo hiki baada ya kuletewa maombi tukaona tujikusanye kwa kila mmoja alichonacho tuje tupaone hapa kituo cha Zimamusalikin. 

 

 Tumekuja tunayo yale ambayo tumeayapata yawezeka kikawa ni kidogo ila ssisi tunaona ni kikubwa nma kitawafariji.” Amesema na kuongeza kuwa.


“Bwana Adam hapa ametueleza mahitaji  makuu mawili sasa sisi kwa namna ya pekee tutaanza taratibu, tutashirikiana kwa pamoja ili tuweze kuona kipi tunaweza kuanza kwa taratibu. Yale ambayo tumeyaletea mtayaona na kuyafurahia, Tumshukuru Mungu kila muda kila wakati na haya huwa yanatuletea majibu.” Amesema Badru Idd.

Kwa niaba ya wananchi wa Tandika Diwani wa Kata hiyoUzairu Athumanamesema “niiseme machache, kwanza kabisa nianze kwa kuwashukuru CRDB Benki kwa kuja kuungana nasi wananchi wa Tandika kutoa kichache mlichonacho ni jambo kubwa la kujivunia , bahati nzuri ndugu mgeni rasmi nimekuwa hapa Tandika kwa miaka sita na kata hii ina matawi sita ya benki yenu.


“Naupekee wa hili ambalo Mgeni Rasmi la kuletwana wafanyazi wa crdb benki kwa kutenga   cha kidogo walichonacho wakatenga sehemu kuja kuhudumia sehemu ya watanzania hasa vijana yatima wa kituo hiki mungu awabariki sana.

 
“Niseme mmeisaidia serikali lakini mmeisaidia jamii ya watanmzania, Wilaya temeke kufikia mwaka jana kwa kila siku moja wanazaliwa watoto 100 takwimu za mwaka jana na watoto hao ni wale waliozaliwa hospitali acha wale ambao hawazaliwi hospitalini. Kuja kwenu hapa mmemsaidia Mhe Samia lakini pia mnatusaidia sisi viongozi.” Amesema Athuman.


Mwenyekiti wa kituo hicho Salikini Adam Matembelela Akitoa taarifa fupi ya kituo hicho amesema kituo hicho kilianziashwa mwaka 2014 na Shekh Ahmad Ally, kituo kilianza na watato 11 na sasa kituo kinawatoto 102, wasichana 32 na wavulana 70. Lengo kuu la kituo ni kufundisha na kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.


“Wakati wa kuanzishwa kwa kituo hiki mzee mwenyewe alikuwa msimamizi mkuu wa kituo na uendesghaji wa kiuchumi  kutokna na vyanzo vyake hadi alipofariki 2016 na sisi tukaona si vyema kukivunja kituo hiki hivyo tukachukua jukumu hili la kuwakllea kuanzia hapo hadi sasa.


“Mafanikio ya kituo hiki ni kuwatoa walimu katika kituo hiki, tunao vijana nane mpaka 10 ambao ni waalimu katika taaisi mbalimbali za kidini wakiendelea kufundisha neno ama jina la Mwenyezi Mungu. Lakini pia tunao Maimamu katika misikiti mbalimbali huku wengine wamekuwa walezi wa wenzao katika kituo hiki.


“Changamoto kubwa kuu mbili, kwanza tunayokutana nayo ni udogo wa eneo, eneo letu ni dogo kwa sababu tunatamani kuchukua watoto wengi zaidi hawa 102 tunaona bado lakini eneo letu tunakosa pa kuwaweka wengine ambao tunaamini wanahitaji malezi.


“Changamoto ya pili ni katika chakula, Malazi, mavazi lakini gharama za masomo, watoto hawa wamegawanyika ngazi ya masomo mbalimbali wapo wa kidato cha tano, kidato cha nne waliopo shule ya msingi na waliopo chekechea.” Amesema

No comments:

Post a Comment

Pages