HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2024

SERIKALI YATIA MIGUU YOTE SIMBA NA YANGA CAF CL

NA JOHN RICHARD MARWA

Wakati miamba ya Tanzania katika medani zasoka Klabu za Simba na Yanga zikikwea anga za kimataifa katika michezo ya mkondo wa pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL, Ambapo Mnyama anamfuata Al Ahly jijini Cairo Misri na Yanga wakitua jiji la Pritoria Afrika Kusini kuwavaa Mamelodi Sundowns.

Simba wanaenda kuwakabili Ahly wakiwa nyuma kwa bao moja waliloruhusu nyumbani Benjamin Mkapa ijumaa iliyopita wakati Yanga wakienda na tahadhari kutokana na kutopata matokeo nyumbani walipokubali suluhu jumamosi iliyopita.

WAkati miamba hiyo ikila mwewe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba, ametoa maelekezo mahsusi kwa ofisi za Balozi za Tanzania nchini Afrika Kusini na Misri kuhakikisha zinatoa msaada wowote utakaohitajika kwa timu za Simba na Yanga zitakapokuwa katika nchi hizo mwishoni mwa wiki.

Simba na Yanga zinawania kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba wanahitaji kushinda kuanzia mabao mawili ili kuwaondoa Ahly, wakati Yanga wakienda na miguu miwili kupata ushindi ama sare ya mabao moja kwa moja watakuwa wanatinga hatua inayofuata. 

Ni kutokana na umuhimu wa mechi hizo, waziri Makamba kupitia ukurasa wake wa X zamani ukijulikana kama Twitter, amesema tayari amezielekeza ofisi za ubalozi katika nchi hizo kuhakikisha zinazipa timu hizo kila aina ya ushirikiano ili zipate ushindi ugenini.

"Balozi zetu za Pretoria na Cairo zimeelekezwa kutoa msaada wote kwa timu zetu za Simba na Yanga zitakapocheza huko wiki hii. Timu zitapokewa na mabalozi. Maafisa wetu watakuwa na timu saa zote kuhakikisha mkono wa Serikali upo kwa msaada na kukabili changamoto. Tunazitakia heri," ameandika waziri Makamba katika ukurasa wake huo leo Aprili 1,2024.

No comments:

Post a Comment

Pages