Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, (wapili kushoto), akikabidhi moja ya zawadi kwa Watoto wenye mahitaji maalum, wanaolelewa katika kituo cha Safina Jijini Dodoma, kwa niaba ya wafayakazi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar walipotembelea katika vituo hivyo na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo fedha, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine muhimu kama sehemu ya kukamilisha Tamasha la Pasaka mwaka 2024.
Na Asia Singano na Chedaiwe Msuya – WF- Dodoma
Tamasha
la Pasaka lililoandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya
Rais Fedha na MipangoZanzibar kwa Mwaka 2024, limehitimishwa baada ya
watumishi wa Wizara ya Fedha pande zote mbili za Muungano kukamilisha
zoezi la kutoa misaada kwa vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji
maalum na vituo vya watoto yatima.
Akizungumza
katika hafla ya kuagana na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa’ Golden Crown’ jijini Dodoma,
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha,
Bw. Lusius Mwenda, aliwashukuru watumishi wote wa pande zote mbili kwa
ushiriki wao katika Tamasha hilo huku akiahidi kufanyika kwa tukio kama
hilo mwakani.
“Nimefurahi
sana na nawashukuru kwa ushiriki wenu, msafiri salama na endapo
kutakuwa na changamoto yoyote tunaomba mtufahamishe, tuna ofisi sehemu
mbalimbali ikiwemo Dar Es Salaam na maeneo mengine hapa nchini hivyo ni
rahisi kusaidia ikiwa kutatokea changamoto yoyote ‘’ Alisema Bw. Mwenda
Kwa
upande wake, Afisa Uendeshaji kutoka Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango
Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumzia kuhusu ziara ya kutembelea vituo
vya watu wenye uhitaji, aliainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili
watu wenye mahitaji maalum na vituo vya kulelea watoto yatima ikiwemo
makazi na fedha za kujiendesha.
‘’Tumeona
changamoto nyingi za vituo hivi mfano kituo cha Safina kina uhitaji wa
pampu za kusukuma maji ambazo matengenezo yote yanagharimu kiasi cha
shilingi milioni saba na nusu na tumewapa milioni moja tu’’ alisema Bw.
Uweje
Aliongeza
kuwa Ofisi ya Rais Fedha na Mipago Zanzibar itashirikiana na Wizara ya
Fedha Tanzania Bara ili kuona namna ya kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili watu wenye mahitaji maalumu katika vituo hivyo katika
awamu nyingine.
"Na
tumetoa ahadi kuwa tumechukua zile changamoto zao ili tuone tunaenda
kuzifanyia kazi vipi, endapo tutafanikiwa kuwa mshawishi viongozi wetu
katika Taasisi zetu basi tutarudi na kuona tutawasaidia vipi"Aliongeza
Bw. Uweje.
Aidha,
alitoa wito kwa walezi wanaohudumia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo
Watoto yatima kuwalea katika malezi bora ili wasione utofauti na watu
wengine ikiwa ni pamoja na kuwasimamia katika masomo yao na kuwapa
misingi bora ya kiimani kwa kila mmoja kutokana na dini yake.
"Wito
wangu kwa walezi wa vituo waendelee kuwatunza watoto hawa, kuwasimamia
vizuri ili muwe na mchango bora kwa Taifa na raia wema wa leo na baadae"
alisisitiza Bw. Uweje.
Kila
mwaka Watumishi wa Wizara ya Fedha na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha
na Mipango Zanzibar hutembelea vituo mbalimbali na kufanya matendo ya
huruma katika maeneo yote mawili kwa zamu (Tanzania Bara na Zanzibar)
ambapo kwa mwaka huu wametembelea Vituo vya Safina, Asmaa Bint Shams
kilichopo kisasa, kituo cha watu wazima (wakubwa) wasioona Buigiri na
Kituo cha Watoto wenye uhitaji maalum kilichopo Shule ya Msingi Buigiri
na kutoa misaada ya vitu mbalimbai ikiwemo vyakula, sabuni, mafuta, dawa
za meno, fedha na mahitaji mengine.
No comments:
Post a Comment