Afisa maendeleo ya Michezo wa Manispaa ya Morogoro, Johnerick Fredirick(kulia) akimkabidhi Melkizedeck Amedeus kikombe mara baada ya kuibuka bingwa wa mashindano ya Pasaka mchezaji mmoja mmoja(Singles) yajulikanayo kama “Star Park Easter Grand Open Pool Competitions 2024” yaliyomalizika mkoani Morogoro.
Na Michael Machela
TIMU ya mchezo wa Pool ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani Kinondoni jijini Dar es Salaam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano Pasaka yaliyojulikana kama “Star Park Easter Grand Open Pool Competitions 2024” kwa kuifunga timu ya Masti yenye makazi yake Posta Ilala jijini Dar es Salaam 13 – 8 na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi milioni moja.
Mshindi wa pili ni timu ya Masti ambayo ilizawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano.
Mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni timu ya Skylight yenye makazi yake Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam ambao walizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja na mshindi wa nne ni Shani Cinema na Morogoro ambao walizawadiwa shilingi elfu hamsini.
Mashindano hayo yalikuwa na mchezaji mmoja mmoja(Singles) ambapo Melkizedeck Amedeus kutoka timu ya Snipers aliibuka kuwa bingwa kwa kumfunga Seif Hamadi 7 – 5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano.
Seif Hamadi alichukuwa nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa shilingi laki mbili.
Mshindi wa tatu mchezaji mmoja mmoja ni Patrick Nyangusi ambaye alizawadiwa shilingi laki moka na mshindi wa nne ni Festo Yohana ambaye alizawadiwa shilingi elfu hamsini.
No comments:
Post a Comment