HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2024

TAKUKURU YAFANIKISHA MAREJESHO YA SH.MILIONI 439.2 KUTOKA KWA WANUFAIKA WA MIKOPO ASILIMIA 10 JIJI LA TANGA

 

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga Victot Swella akizungumza na waandshi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 ambapo alisema kwamba moja ya kazi walioifanya ni ufuatiliaji wa ufanisi katika utekelezaji mkakati wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga Victot Swella akizungumza na waandshi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 ambapo alisema kwamba moja ya kazi walioifanya ni ufuatiliaji wa ufanisi katika utekelezaji mkakati wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.


Na Oscar Assenga,TANGA.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani Tanga imefanikisha marejesho ya kiasi cha Sh. Milioni 439,279,300.00 kutoka kwa wanufaika wa mikopo asilimia 10 katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga Victot Swella wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwaa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 ambapo alisema kwamba moja ya kazi walioifanya ni ufuatiliaji wa ufanisi katika utekelezaji mkakati wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Alisema kwamba miongoni mwa changamoto waliozozibaini katika ufuatiliaji huo ni kutokuzingatiwa kwa masharti ya urejeshaji mikopo hiyo kwa wakati kutoka kwa wanufaika ambapo kabla ufuatiliaji kufanyika kiasi cha Bilioni 2,152,229,900 zilikuwa hazijarejeshwa kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo na muda wa marejesho ulikuwa umeshapita.

Aidha alisema baada ya kulibaini hilo taasisi hiyo iliwakutanisha wadau na kuweka mapendekezo ya kurejesha fedha hizo na hadi kufikia mwezi Februari 2024 Jumla ya Sh.Milioni 439,279,300.00 zilikuwa zimerejeshwa katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na kufanya fedha ambazo hazijarejeshwa kuwa ni Bilioni 1,712,950,600.00 huku jitihada za ufuatiliaji zinaendelea.

Mkuu huyo wa Takukuru alisema pia katika kipindi hicho walifanikiwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Bilioni 8,041,998,680.00 katika sekta za kipaumbele kama vile elimu,barabara ,maji na afya.

Alisema katika ufuatiliaji huo walibaini miradi 32 yenye thamani ya Bilioni 4,866,068,966.00 kuwa na mapungufu na ushauri ulitolewa wa kurekebisha mapungufu hayo kupitia vikao na wadau husika pamoja na kuanzisha uchunguzi wa miradi ambayo walibaini uwepo wa tuhuma za vitendo vya rushwa.

“Miongoni mwa miradi tunayoichunguza katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe ni manunuzi ya Sh. Milioni 6,400,000 ya uwekaji milango kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara wenye thamani ya Milioni 245 lakini pia ujenzi wa madarasa mawili ,matundu 18 ya vyoo na mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua wenye thamani ya Milioni 70,000,000 na uchunguzi unaofanyika ni wa ubadhirifu wa Sh.Milioni 30,000,000.00 kwenye ujenzi wa matundu hayo ya vyoo na mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua.

No comments:

Post a Comment

Pages