May 18, 2024

Mabalozi, Wanadiplomasia kushiriki Afrika Marathon Maadhimisho ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika Mabalozi zaidi ya 62 na Wanadiplomasia wanatarajia kushiriki Mbio za Afrika Marathon za Kilometa 5 hadi15 zinazotarajia kufanyika Mei18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ally Bujiku amesema kuwa mbio hizo zitafanyika kuelekea kuadhimisha  miaka 61ya maadhimisho ya umoja wa nchi hizo na kwamba zina lengo la kukuza Diplomasia katika sekta ya michezo.

"Michezo ni biashara,ni ajira ni kazi pia ni Diplomasia,tumechagua riadha kwasababu kila mtu anaweza kushiriki" amesema  Balozi Bujiku.

Amebainisha kuwa mbio hizo zitaanzia katika Daraja la Tanzanite, Mtaa wa Barrack Obama hadi Masaki na kwamba fedha zitakazopatikana zitapelekwa Shule za Wanafunzi wenye mahitaji maalum. 

Amesisistiza kuwa mabalozi watatoa misaada katika shule hizo huku akiwahimiza wananchi kushiriki kwa wingi kufanikisha maadhimisho hayo.

Ameongeza kuwa baada ya Marathon Mei 20 mwaka huu washiriki wote wa mbio za maadhimisho hayo watashiriki chakula cha jioni cha pamoja katika Hoteli ya Serena.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo, Balozi Mindi Kasiga  amesema mbio hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa wanariadha wakongwe akiwemo Juma Ikangaa.

Balozi Mindi amefafanua kuwa shule zitakazopata misaada itakayotolewa kuelekea maadhimisho hayo ni Pugu, Uhuru Mchanganyiko pamoja na Shule ya Sekondari  Jangwani.

Pia amesema Mei 25, 2024 ambapo ndio kilele cha maadhimisho hayo Tanzania italipokea Baraza la Amani na Usalama 

Nae, Balozi wa Kenya Nchini Tanzania, Isaac Njenga amesema kuwa atashiriki mbio hizo kwani zina umuhimu mkubwa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa nchi za Afrika

Balozi wa Somalia Nchini Tanzania, Yassini Ally khali amesema yupo tayari kukimbia kilometa 15 zitakazoanzia Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere hadi Masaki.

 



No comments:

Post a Comment

Pages