Mjumbe wa Kamati Kuu Chama cha ACT Wazalendo Mansour Yussuf Himid amesema kuna umuhimu mkubwa kuendelea harakati za kudai mabadiliko ya uongozi Zanzibar kwani chama kinachoendelea kutawala sasa hakina dhamira njema kwa wananchi wa Zanzibar bali wapo kwa ajili maslahi yao binafsi.
Mansour ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa
chama hicho uwanja wa kivumbi Shehia ya Kwamtipura, Jimbo la Shauri Moyo
Mjini Unguja.
Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi wa
Zanzibar kuendelea kushikamana bila kujali maslahi ya chama na badala
yake wakichague chama cha ACT Wazalendo ili kiongoze Zanzibar kwa
misingi ya kisheria na matakwa ya walio wengi.
Amesema kwa muda
wote wa utawala wa Chama cha Mapinduzi awamu hii inayoongozwa na
Dkt, Hussein Ali Mwinyi imekithiri rushwa na uhujumu wa uchumi huku
wanaofanya hayo wakishindwa kuchukuliwa hatua yoyote hile.
Amesema
kwa sababu ya kukosa misingi imara ya uongozi kwenye chama hicho CCM
wameamua kuwawekea chuki wale wote wasiokiunga chama chao na kuwakosehs
ahaki za msingi zikiwemo za kupata vitambulisho pamoja na nafasi za
ajira.
‘’Hii ni dalili mbaya sana ukiona kiongozi anaogopwa
kusemwa maana yake hana uadilifu na lazima wajue wazee wetu wamepindua
ili tuishi kwa upendo na mshikamano sio wanavotufanya wao
tuishi’’alisema Himid.
Sambamba na hayo alisema wazanzibar
wanapaswa kufahamu kuwa Chama cha Mapinduzi CCM hakijawahi kushinda
Uchaguzi hata mmoja Zanzibar awamu zote na kueleza kuwa chini ya Rais
Mwinyi ACT wazalendo itashinda kirahisi mnoo.
Kwa upande wake
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema
wataendelea kufanya kazi za siasa wakiamini kuwa wananchi wa Zanzibar
wamechoshwa na ugumu wa maisha uliosababishwa na CCM.
Pia Jussa
ameshangazwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuendelea kuhubiri
vitisho kwenye mikutano yao na kueleza kuwa kufanya hivyo ni kuishiwa
sera na ndio maana wanahubiri chuki na sio kufanya kazi za siasa.
“Wacheni kufanya vitisho kwa wananchi watu washawakataeni na nilazima 2025 tuwaondoe kwa nguvu ya wananchi” alieleza Jussa.
Ameeleza
na mipango mibovu ya Serikali inayoongozwa na CCM leo wafanyakazi wote
ambao ni waajiriwa wana hali duni sana ya maisha.
Amefahamisha
kuwa kwa sababu ya mazingira hayo imefika wakati waajiriwa wa Serikali
wanawekeza malengo yao kwenye pesa ambazo watalipwa baada ya kustaafu
kazi wakati ambao hawana nguvu tena ya kufanya lolote na baada ya muda
mfupi hufariki Dunia kwa sababu ya msongo wa mawazo.
Alisema
kutokana na utawala huu ambao haujali maslahi ya wananchi inasikitisha
sana katika tawala zote zilizowahi kupita, Zanzibar haijawahi kuwa na
deni kubwa zaidi kuliko awamu hii inayoongozwa na Dkt,Hussein Ali
Mwinyi na kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hadi sasa
Zanzibar inadaiwa shilini trilioni 1.1 kiasia ambacho hakijawahi kutokea
kwa awamu zote.
Alisema Serikali iliyopo madarakani imekuwa ikikopa mpaka benk za ndani na kupelekea kudai kila pembe ya Dunia.
Alisema
kiwango hichi kikubwa cha deni ni kukosekana kwa misingi bora ya
uongozi pamoja na ufisadi mkubwa unaofanywa kila leo huku wanaofanya
licha ya kutajwa kwao katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
hesabu za Seriukali (CAG) hakuna kinachofanyika kwa wanaotenda hayo
wakishindwa kuwajibishwa.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo
mjumbe wa Kamati Kuu Shuena Faki Haji amesema kuwa kwa muda mrefu
Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakibaguliwa kwa itikadi za kisiasa jambo
ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Alieleza kuwa kwa sababu
watawala waliopo madarakani wamekuwa wakijali sana matumbo yao na
familia zao huku wakiwacha wengine katika hali ngumu za kimaisha.
No comments:
Post a Comment