HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2024

DC MAGOTI ASHIRIKI MAZISHI YA MWENYEKITI WA BAMITA

NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
 
Mkuu mpya  wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Petro Magoti  leo Jumamosi ameungana na mamia ya  wananchi wake wa kutoka sehemu mbali mbali za Kisarawe kwa ajili ya kushiriki mazishi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA).

Marehemu mzee Salumu Sung'e salumu ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa kamati ya amani ya Wilaya ya Kisarawe  alifariki siku ya  jana Mkoani na mazishi yake yamefanyika kijiji cha Mengwa kata Boga na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Kisarawe.

Akitoa salamu za rambi rambi katika msiba huo Mkuu wa Wilaya hiyo petro Magoti ameelezea mambo makubwa na mazuri aliyoyafanya marahemu  Mzee Salumu katika enzi za uhai wake akiwa  katika nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya amani katika Wilaya ya Kisarawe na nafasi mbali mbali za uongozi.

Mkuu huyo wa Wilaya  aliwaomba wananchi wa Kisarawe  kuhakikisha kwamba wana muhenzi kwa heshima  mzee huyo na kuwaomba kuweka misingi mizuri kwa ajili ya kudumisha amani na upendo  na kumpa ushirikiano  wa kutosha katika shughuli mbali mbali zinazofanyika katika Wilaya  ya Kisarawe.

Kadhalika alifafanua kwamba kwa  niaba ya Serikali ya  Wiaya ya Kisarawe ametoa pole nakusema Serikali ipo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na huzuni kubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia  nzima.

Pia katika mazishi hayo Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mh. Seleman Jafo ambaye pia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais muungano na mazingira naye ameshiriki kikamilifu na wananchi wa jimbo lake katika mazishi hayo na kuwafariji wafiwa wote ambao wameondokewa na mzee huyo ambaye alikuwa ni kiongozi wa kuigwa.

Waziri Jafo alisema kwamba marehemu wakati wa uhai  wake alikuwa ni mtu shupavu na imara na alikuwa mwenye kutekeleza majukumu yake ya kazi ipasavyo  na kwamba atamkumbuka kwa yale yote mazuri ambayo ameweza kuyafanya kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine.

"Kwa kweli mzee wetu nimekuwa nae kwa kipindi kirefu sana na tumeweza kufanya naye kazi kwa umoja kwa kipindi chote kwa hivyo natoa pole nyingi sana kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mzee wetu na kitu kikubwa tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampokee na apumzike salama,"alisema Waziri Jafo.


Katika mazishi hayo pia wamehudhulia viongozi mbali mbali wakiwemo wa chama cha mapinduzi wakiongozwa na mwenyekiti wao Halfani Sika, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kisarawe, viongozi mbali mbali wa madhehebu ya dini, wakuu wa idara pamoja na wananchi kutoka maeneo ya Kisarawe na maeneo mengine ya jirani ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages