Na Mwandishi Wetu,
Wapiga kura 11,936 wanatarajiwa kupiga kura kesho tarehe 09 Juni, 2024 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo tarehe 07 Juni, 2024
jijini Dar es Salaam wakati akisoma risala kwa ajili ya uchaguzi huo na
kuongeza kwamba uchaguzi utahusisha vituo 29 vya kupigia kura.
“Jumla ya wapiga kura 11,936 walioandikishwa katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
watashiriki katika uchaguzi huu mdogo na jumla ya vituo 29 vya kupigia kura
vitatumika,” amesema Jaji Mwambegele.
Wagombea wanaowania Kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani
majina yao na vyama katika Mabano ni Bw.
Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makaini), Bi. Nuru Abdulla Shamte (DP),
Bi. Mwanakombo Hamad Hassan (NLD), Bi. Zainab Maulid Abdallah (CCK), Bi. Tatu
Omary Mungi (UPDP), Bw. Khamis Yussuuf Mussa (CCM) na Bi. Jarade Ased Khamis
(AAFP).
Wengine ni Bw.
Kombo Ali Juma (NRA), Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad
(UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi.
Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).
Mwenyekiti wa Tume amevikumbusha vyama vya siasa,
wagombea, mawakala wa vyama, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuhakikisha
kwamba hawapigi kampeni siku ya kupiga kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume
cha sheria.
“Alama za vyama
vya siasa zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi
haviruhusiwi kutumika kesho tarehe 08 Juni, 2024 ambayo ni siku ya uchaguzi,”
amesema.
Jaji Mwambegele ameongeza kwamba zoezi la kupiga kura
katika maeneo yote ya uchaguzi litafanyika katika vituo vilevile vilivyotumika
wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Ameongeza kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa
saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.
“Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura
katika mstari ambao wamefika kabla ya sa…
WAPIGAKURA 11,936 KUPIGA KURA KWAHANI
Wapiga kura 11,936 wanatarajiwa kupiga kura kesho tarehe 09 Juni, 2024 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akikabidhi nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kwa viongozi na wawakilishi wa Vyama 19 vyenye usajili kamili wakati Vyama hivyo vilipokutana katika mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.
Mapema wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Jaji Mwambegele aliahidi kuvipatia nakala hiyo vyama vyote na pia Vyama hivyo vitapatiwa nakala tepe ya orodha hiyo.
“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha Kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.
Vyama hivyo vilivyopokea ni AAFP, ACT - WAZALENDO, ADA - TADEA, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CHAUMA, CUF, Demokrasia Makaini, DP, NCCRA- MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.
No comments:
Post a Comment