Kikosi cha Simba Queens kilitwaa ubingwa wa makala ya nne ya Ligi Kuu Soka ya Wanawake mara baada ya kuwafunga Alliance Girls kwa mabao matatu kwa mtungi.
Simba Queens wametwaa ubingwa walioupoteza msimu uliopita mbele ya JKT Queens na sasa wanakuwa Mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Wanawake wakitwaa mara nne huku JKT Queens wametwaa mara tatu na Mlandizi Queens mara moja toka kuanzishwa kwa Ligi hiyo.
Simba Queens kwa ubingwa huo wanapata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF WCL ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo wakitwaa ubingwa watafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF WCL msimu ujao.
Ikumbukwe kuwa Simba Queens msimu juzi walishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kuishia nafasi ya nne baada ya kuondoshwa hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Ni mafanikio kwa kikosi kilichoanza msimu chini ya kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda!a na Musa Hassan Mgosi, kabla ya Mgunda kupelekwa kwa timu ya wanaume kumalizia msimu ambapo wameishia nafasi ya tatu nyuma ya Mabingwa Young Africans SC na Azam FC.
Wakati upepo mbaya ukiwa umetanda mitaaa ya Msimbazi, Simba Queens wao waliziba masikio na kufanya kazi waliyotumwa msimu huu ya kurejesha furaha kwa wanasimba kwa kutwaa ubigwa huo wa Ligi ya Wanawake
No comments:
Post a Comment