Na John Richard Marwa
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Young Africans Miguel Angel Gamondi ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja kusalia katika klabu hiyo msimu ujao wa mashindano 2024/2025.
Hayo yamejiri katika mkutano Mkuu wa klabu ya Yanga ambao umefanyika leo kujadili mambo mbalimbali ya klabu hiyo baada ya msimu kumalizika.
Pamoja na ajenda mbalimbali moja ya jambo kubwa ambalo limefunga mkutano huo ni uwepo wa Kocha Miguel Gamondi na yeye kuthibitisha kuwa atasalia mitaa ya Twiga na Jangwani kwa msimu mmoja ujao na tabu iko palepale.
Gamondi alijiunga na Mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania msimu uliopita aikipokea mikoba ya Nasriddine Nabi na kufanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL, CRDB Federation Cup, kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL baada ya miaka 25, kuongeza namba za pointi kwenye Ligi, namba za mabao ya kufunga na kupunguza mabao ya kufungwa.
Swali ni je Angel Gamondi atafanikiwa kutetea mataji aliyoyachukua msimu uliomalizika na kuchukua mengine kama Ngao ya Jamii ambayo waliipoteza, huku akiwa na kibarua cha kuipeleka hatua za mbele zaidi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL? Muda utaamua kama kweli tabu iko palepale ama laaah!.
No comments:
Post a Comment