Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua kampeni ya uelewa kuhusu kuanza kwa huduma za usafiri wa Treni katika kiwango Cha kimataifa (SGR) zitakazoanza mwisho wa mwezi wa Julai kutoka Dar es Salaam-Dodoma ambapo tayari shirika limechukua hatua kadhaa ikiwemo kuanza safari zake tarehe mwezi Juni14 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2024 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni hiyo ya uelewa kuhusu kuanza kwa huduma za usafiri wa Treni ya umeme SGR yenye kiwango cha kimataifa huku furaha kuu ya kuimba kaulimbiu isemayo 'Twende tukapande Treni yetu, tuitunze, tuithamini'.
"Shirika litaanza kutoa huduma za awali za usafiri wa Treni katika Reli ya kiwango Cha kimataifa (SGR) kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ifikapo tarehe 14 Juni 2024, hii ikiwa ni sehemu ya kuendelea kujifunza teknolojia hiyo mpya nchini na kujiridhisha mifumo mbalimbali ya uendeshaji huduma za usafiri wa Treni kabla ya kuanza rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam - Dodoma ifikapo tarehe 25 Juali 2024"amesema Mkurugenzi
Wananchi wamesisitizwa kuendelea kushirikiana kutunza miundombinu ya Reli hiyo kwani ni Mali ya watanzania wote imejengwa kwa fedha za walipakodi wa kuanza kwa kutumia huduma hiyo ya usafiri itasaidia kuongeza pato la Taifa.
Hata hivyo wanaotarajia kutumia usafiri huo watahakikishiwa ulinzi na kutosha kuanzia abiria na mizigo kwa ujumla.
"Jambo hili ni muhimu sana ni usalama wa Reli yetu, usalama wa abiria na mizigo, kwani kutakuwa na CCTV Camera tutakua na wataalamu watu ambao watakuwa wanaangalia kila kinachoendelea kwenye treni yetu kwa masaa 24, pia uwepo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama a maaskari ndani ya Treni ambao watasafiri nasi mwanzo hadi mwisho"
"Kwenye miundombinu, pamoja na kufanya doria, stesheni zetu zote zinavituo vya polisi na tunaimani kuwa kutakua na utaratibu wa kuwepo na maaskari huko njiani, pia Askari watafanya doria, tutakua na walinzi watakuwa wanafanya kazi masaa 24"
Sambamba na abiria wanaweza kukata tiketi kwa njia ya mtandao au kupitia madirisha ya kukatia tiketi ndani ya stesheni kwa njia ya mtandao kwani abiria atatakiwa kukata tiketi wiki Moja au siku 3 kabla ya safari ili kuepukana na msongamano.
Kuhusu nauli Kadogosa amesema tayari LATRA wameshatangaza nauli na hivyo wateja wawe tayari kwa safari na gharama iliyowekwa ni rafiki na wananchi mtu yeyote atamudu
"LATRA wametangaza nauli za daraja la kawaida, lakini tutakua na Treni za aina tatu Tereni ya kawaida itakayosimama Kila sehemu, tutakua na Treni za Moja kwa moja (Express) na Treni mchongoko"
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara (TCB) Adam Mihayo amesema katika safari hizo za Reli ya SGR, TCB wameshirikiana na TRC katika kukusanya mapato katika vituo vya kukatia tiketi.
Pia Mihayo amesema Benki ya TCB wameshirikiana na TRC kwa kufanikisha kuleta vichwa vya Treni na mabehewa kutoka Ujerumani.
"Ushirikiano wetu na Reli ya Tanzania unaakisi dhamira yetu ya pamoja ya kuelewa mahitaji ya watanzania na kuchangia katika ukuaji wa amaendeleo ya kiuchumi na mafanikio ya Taifa letu"
"TCB tutaendelea kushirikiana na shirika la Reli Tanzania ili kuhakikisha matarajio ya Mhe. Rais katika mradi huu yanaweza kutimia" Alisisitiza
No comments:
Post a Comment