Ujumbe wa Serikali ya India umekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa
Serikali ya Tanzania, na Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la
Umoja wa Mataifa - FAO Katika Bara la Africa kujadiliana fursa za
ushirikiano baina ya Tanzania na India kwenye nyanja ya uhifadhi wa
Misitu na Wanyamapori.
Rome. Ujumbe wa Serikali ya India
umekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania, na
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa - FAO
Katika Bara la Africa kujadiliana fursa za ushirikiano baina ya Tanzania
na India kwenye nyanja ya uhifadhi wa Misitu na Wanyamapori.
Mazungumzo
hayo yamefanyika jana Julai 24, 2024 katika ofisi za Makao makuu ya
FAO, Rome nchini Italy yaliongozwa na Shri. Jitendra Kumar, Mkurugenzi
Mkuu wa Misitu na Katibu Maalum katika Wizara ya Mazingira, Misitu, na
Mabadiliko ya Tabianchi (MoEFCC) India. Huku Kamishna wa Uhifadhi – TFS
Prof. Dos Santos Silayo ambaye ni makamu mwenyekiti wa Mkutano wa Kamati
ya Misitu (COFO27) na mwakilishi wa Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori
Barani Afrika,akiongoza ujumbe kutoka nchini Tanzania.
Wajumbe
wengine waliohudhuria mkutano huo kutoka India ni maafisa waandamizi
wakiwemo Shri. R. Raghú Prasad, Inspekta Jenerali wa Misitu, na Shri.
Kamal Ject Singh, Naibu Inspekta Jenerali wa Misitu kutoka MoEFCC,
pamoja na Shri Anoop Singh, Mkurugenzi Mkuu wa Utafiti wa Misitu nchini
India na baadhi ya maafisa wa ubalozi wao. Huku Upande wa Tanzania ukiwa
na Dr. Elikana John, Afisa Mwandamizi na Mtalaam wa Misitu, Edward
Kilawe, Mtanzania na Mwakilishi wa FAO Katika Bara la Africa yenye Makao
Mkuu ya Jijini Accra Ghana.
TFS, Prof. Silayo anasema
mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kimataifa katika
kujenga uwezo wa tathmini ya rasilimali za misitu, ikiwa ni pamoja na
upimaji na utafiti wa misitu, uendelezaji wa mfumo wa ufuatiliaji wa
moto wa misitu kwa wakati sahihi, na ushiriki katika Umoja wa Kimataifa
wa Wanyama Jamii ya Paka Wakubwa, unaohusisha Afrika Kusini, Ghana,
Kenya, Zimbabwe, na Namibia.
“Kwa pamoja tumezungumza umuhimu wa
nchi zetu mbili kushirikiana katika uhifadhi ikiwa ni mwendelezo wa
mahusiano mazuri yaliyopo baina yaTanzania na India, kama yalivyotiwa
msukumo na Waheshimiwa Viongozi wakuu wa nchi hizi!
Tumekubaliana
kuanza mazungumzo ya kuiwezesha Tanzania kujiunga na umoja wa nchi
zinazoweka nguvu pamoja kuhifadhi Wanyama jamii ya paka wakubwa
(International Big Cat Alliance). Umoja huu utawezesha nchi zetu
kubadilishana uzoefu, utalaam, teknologia na vifaa vitakavyowezesha
uhifadhi na ufuatiliaji wa misitu na rasilimali za wanyamapori.
Mazungumzo yanaendelea kufanikisha azma hii. Tunaishukuru ofisi ya
Ubalozi wa Tanzania Rome kwa kuratibu mazungumzo hayo.,” amesema.
Mkutano
huo wa pande mbili, uliofanyika kandokando ya kikao cha 27 cha Kamati
ya Misitu (COFO), ulitoa jukwaa kwa pande zote mbili kuchunguza njia za
ushirikiano zitakazonufaisha sekta za misitu na wanyamapori.
No comments:
Post a Comment