Julai 17, 2024 – Serikali Marekani, India, na Tanzania zimeungana kukuza na kuimarisha miundombinu ya nishati mbadala nchini Tanzania. Muungano huu wa kipeke wa nishati safi ni wa kwanza wa katika bara ya Afrika. Ushirikiano huu unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali lenye makao makuu Marekani, ‘The Asia Foundation’, utaboresha uwezo wa kila nchi, na kwa pamoja, kufanya gridi ya taifa kuwa na nguvu zaidi, mifumo ya udhibiti na sera iliyoboreshwa, na muungano wa kikanda imara, pamoja na kuendeleza matumizi ya nishati ya jua nchini Tanzania.
Marekani inaendelea kuwa mshirika mkubwa wa Tanzania na kuharakisha usambazaji wa umeme nchini Tanzania, ili jamii kote nchini ziweze kupata nishati safi na ya uhakika. Tangu mwaka 2013, mpango wa USAID wa Power Afrika ulipoanza, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika sekta ya nishati kwa kuongeza upatikanaji wa umeme kutoka takriban watu milioni 1.2 hadi zaidi ya watu milioni 4.5 mwaka 2023.
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) linashirikiana na Vituo vya Ubora vya India, vikiwemo Grid Controller of India Limited na NTPC School of Business, kuwashirikisha watunga sera, wadhibiti, watoa huduma, wasomi na sekta binafsi nchini Tanzania ili kupanua wigo wa matumizi ya nishati mbadala na kukuza uwekezaji wa nishati inayozingatia tabianchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini Tanzania, Alexander Klaits alisema, “Sasa tunaanza ushirikiano mpya muhimu, pamoja na serikali ya India, unaopanua ushirikiano wa nishati na Tanzania. Ushirikiano huu utaimarisha uwezo wa ndani, na kuongeza fursa za biashara baina ya makampuni ya Marekani nchini Tanzania. Tunayo heshima kushirikiana na serikali ya India kusaidia Tanzania kuendelea kuwa msafirishaji mkuu wa nishati katika kanda ya Afrika Mashariki.”
Balozi Mdogo wa Ubalozi wa India Manoj Verma alisema, “Ni jambo la kujivunia kuona ushirikiano wa kwanza kati ya India na Marekani katika bara la Afrika unafanyika nchini Tanzania. Ushirikiano huu unatoa mfano imara wa kimkakati kati ya Tanzania na India. Kwa kuzingatia maendeleo ya nishati mbadala na usimamizi wa gridi ya taifa, ushirikiano huu utaongeza juhudi za Tanzania inapokaribia kukamilisha miradi mikuu ya nishati na kuunganisha gridi yake na nchi katika ukanda huu. Tuna imani kwamba ushirikiano kati ya nchi hizi tatu utatumia uzoefu mkubwa na India katika Eneo la Nishati Mbadala, kuboresha maisha ya Watanzania kwa njia endelevu.”
Naibu Katibu Mkuu Dr. James Peter Mataragio, Wizara ya Nishati, Serikali ya Tanzania alisema, “Nimefurahi sana kuwa sehemu ya ushirikiano huu. Tanzania itafaidika sana kutokana na uzoefu na mafunzo ya Marekani na India katika kutengeneza nishati ya jua na upepo. Kwa pamoja tunaweza kuchochea maendeleo ya nishati mbadala na gridi ya taifa yenye nguvu zaidi nchini Tanzania.”
No comments:
Post a Comment