HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2024

RC CHALAMILA; WANANCHI WA DAR ES SALAAM JITOKEZENI KUPIMA HOMA YA INI NA KUPATA CHANJO

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Wizara ya Afya kupitia Mpango wake kabambe wa kudhibiti  Ukimwi magonjwa ya ngono pamoja na homa ya Ini kwa kushirikiana na Mkoa wa Dar es salaam wamewashauri wananchi kujitokeza kupima kupima  homa ya Ini na kupata chanjo.


Wito huo umetolewa leo Julai 25 ,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Abert Chalamila katika maadhimisho ya homa ya Ini Duniani ambayo hufanyika Julai 25 hadi 28 Mwaka huu ambapo kwa Mkoa huo yatafanyika katika viwanja vya Sinza Darajani Ubungo kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi jioni .

"Homa ya ini ni ugonjwa hatari sanaa nawasihi wakazi wangu wa mkoa huu jitokezeni kwa wingi mkutane na madkatari bingwa kutoka hospitali zetu pia kutakuwa na upimaji magonjwa mengine na ushauri nasaha utatolewa mambo kadhaa kuhusiana na namna bora ya kuishi ili mtu asiugue homa ya ini" amesema Chalamila

Sambamba na hayo amebainisha kuwa siku hizo kitakachofanyika ni upimaji ini utoaji chanjo na ikiwa mtu tayari atakuwa amepatikana na ugonjwa huo atachangia kiasi cha fedha ili apatiwe tiba na atapona kabisa .

Kwa upande wake Mkurugenzi huduma tiba Hospitali ya Taifa Mhimbili Dkt John Rwegasha amesema Mtu anaweza kuishi na virusi vya homa ya Ini zaidi ya mika 20 pasipo kutambua na ugonjwa huo huwa ni wa  kimya kimya lakinj madhara yake ni muda mrefu ya kwani ukija ghafla huweza kuibuka na kansa ya ini hivyo ni vyema watu kujitokeza kupima na kupata chanjo.

"Tatizo hili hili ni kubwa Kidunia hata kinchi na takwimu iliyofanyika 2022 Tanzania tulikuwa 4% na kidunia tuko kwenye ukanda 8%  hii inaonyesha kuwa watu milioni 60 ni watu milioni 2 tu ndiyo wanaoishi na virusi vya homa ya ini " amesema Dkt John

Hata hivyo Dkt amefafanua kuwa homa ya ini ina makundi 5 ya virusi A,B,C,D,E,  ambao virusi kundi A na E huambukizwa kwa njia ya mfumo wa chakula kunywa maji ambayo si masafi na vyakula ambayo si salama husababisha tumbo kuuma ,kuharisha B na C yenyewe huambukizwa kwa njia ya damu kuchangiana vitu vya ncha kali ikiwemo viwembe baadhi yao hupata wakiwa watoto na maambukidhi ya B yanatokana na afya ya mama na mtoto na mtoto akipata huishia na virusi hivyoa hadi miaka 30 na kuanza kupata magonjwa nyemelezi hivyo kupitia mpango huu kabambe wananchi ni vyema kujitokeza kupima na kupata tiba na chanjo mapema.

Aidha katika kilele cha Maadhimisho hayo julai 28, mwaka huu Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu anatarajiwa  kuhitimisha  hivyo kauli mbiu "ni wakati wa kuchukua hatua kwa vitendo"


No comments:

Post a Comment

Pages