Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amezindua Jengo la Kisasa la Kitengo cha Usafishaji wa Damu (Dialysis) katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke (TRRH) ambalo litakuwa likitoa
huduma na matibabu ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo.
Hafla
ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo ndani ya hospitali hiyo Jijini Dar
es Salaam imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali
wa serikali na sekta binafsi.
Akizungumza
baada ya uzinduzi wa jengo hilo kwa niaba ya Waziri wa afya Ummy
Mwalimu, Mkuu wa wilaya hiyo amesema uwepo wa kituo hicho utapunguza
msongamano wa wagonjwa wanaokwenda hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kupata huduma ya kusafisha damu(dialysis)ambapo hospitali hiyo Pekee
ndiyo iliyokiwa ikitoa huduma hiyo hapo awali.
"Nadhani
sasa ujio wa Jengo hili ambalo Lina vifaa vya kisasa Kanisa litatoa
matibabu ya huduma za dialysis siyo tu kwa wakazi wa Temeke pekee bali
mpaka wale wanaokwenda kuifuata huduma hiyo hospitali ya Taifa ya
Muhimbili hivyo niwapongeze wadau kwa kutoa michango yao ya Hali na mali
hasa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) "amesema.
Uzinduzi
wa Jengo la kusafisha damu ndani ya hospitali hiyo ambalo lina vifaa
vya kisasa vya kutoa huduma ya usafishaji wa damu pia umeenda sambamba
na Uzinduzi wa Gari la kubeba Wagonjwa (Ambulance) pamoja na Basi la
kubeba watumishi wa hospitali hiyo katika kutekeleza majukumu yao kwa
ufanisi zaidi.
Akizungumza
kuhusu magonjwa yasiyoambukiza DC Mapunda amebainisha kuwa tafiti na
tathmini zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile
Shinikizo la Damu,Sukari,pamoja Afya ya Akili yamekua yakiongezeka
kutokana na ulaji usio faa na kutokufanya Mazoezi hivyo niwakati sasa
wananchi washiriki kufanya Mazoezi na kuacha kula vyakula vyenye Chumvi
Nyingi na Sukari Nyingi,Pombe kupita kiasi pamoja na Matumizi ya
Tumbaku.
"Serikali
imeanza kutekeleza Afua mbalimbali ili kukabiliana na Magonjwa haya
ikiwemo kufanya uratibu jumuishi wa wagonjwa kuanzia ngazi za zahanati
pamoja na kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia wataalamu wa Afya ili
kusaidia kukabiliana na Magonjwa haya ambayo yamekua tishio kubwa kwa
sasa"amesema DC Mapunda
Awali
akitoa taarifa za Utoaji huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro amesema kuwa
Hospitali hiyo toka kuanzishwa kwake mwaka 1970 imepata mafanikio
Makubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili kama
vile Ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo kwa ajili ya kuongeza miundombinu
ya utoaji wa huduma kwa Wananchi.
"
Tumepata mafanikio makubwa sana kwa sasa tunalaza wagonjwa miambili
hamsini(250)hadi mia tatu(300) kwa siku,huku wagonjwa wa nje (OP) ni
zaidi ya elfu mbili, hivyo kituo hiki cha kusafishia Damu tunachozindua
leo tumepata msaada kutoka kwa wenzetu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (
TPA) ambapo wametoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni miambili kwa
ajili ya ukarabati mkubwa wa Jengo la kuweka Mashine,pamoja na shilingi
milioni Kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kama vile Viti
mwendo(Wheelschair? pamoja na vifaa vya Kusafishia Damu" amesema Dkt
Kimaro.
Nakuongeza
kuwa "Tunaomba Wadau wengine wajitokeze kutusaidia ili tuweze
kuboresha huduma za Wananchi wetu na kumuunga Mkono Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan ambaye kwa miaka mitatu ya uongozi wake amewekeza pakubwa
kwenye Sekta ya Afya na wananchi wanapata huduma salama.
Mbali
na hayo pia Mganga Mkuu huyo aliiomba serikali kuwapatia eneo ambalo
wameliomba au kuwapatie eneo lingine kwa ajili ya kuongeza idadi ya
majengo ya hospitali kwani kwa sasa kuna ufinyu wa eneo.
No comments:
Post a Comment