Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam
SHIRIKA la Reli Nchini (TRC) Limekiri kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya abiria wa Treni ya umeme (SGR) kwa kukata tiketi za kushuka njiani na baadae kupitiliza vituo wanavyopaswa kushuka ikiwa ni nje ya thamani ya fedha zao.
Akizingumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk amesema hivi karibuni walipokea taarifa kutoka kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwa kuna abiria wanafanya udanganyifu huo hivyo TRC imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa tiketi.
"Eneo utakalopandia treni utascan tiketi yako,ndani ya treni pia wakaguzi wanafanya ukaguzi wa tiketi wakati wa kushuka unatakiwa kuscani ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote, kama itakuwa kuna abiria kafanya udanganyifu basi alarm zitapiga kelele hivyo walinzi watakuja kuangalia kuna shida gani na wakimbaini sheria kali itachukuliwa dhidi yake".
Hata hivyo ameongeza kuwa Abiria hususani wanaopanda katikati ya safari kuanzia stesheni ya ruvu na ngelengele ndio wengi wanafanya udanganyifu huo ambapo TRC kwa kushirikiana na vyombo vya usalama tayari wamewakamata baadhi yao na kuwafikisha Mahakani,Pia katika sakata hilo TRC imewakamata watu kadhaa waliokuwa wanakata tiketi nyingi kwa wakati mmmoja na kwenda kufanya udanganyifu.
Jamila ameongeza kuwa kwasasa ili kupanda treni ya SGR ni lazima uwe na kitambulisho chochote kinachoonesha sura ya muhusika na jina lake kamili.
Aidha amewataka abiria kuwa waadilifu kwa kulinda mali ya umma na kuhakikisha kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuwafichua wanaohujumu na kusisitiza kuwa kwa yoyote atakayebainika kuhujumu shiriaka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
August 16, 2024
Home
Unlabelled
TRC KUIMARISHA MIFUMO DHIDI YA UDANGANYIFU WA TIKETI
TRC KUIMARISHA MIFUMO DHIDI YA UDANGANYIFU WA TIKETI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment