HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 13, 2024

Hanspaul Group yaipongeza Serikali kuwathamini Wawekezaji wa Ndani, yaja na Magari ya Umeme kuunga Mkono Matumizi ya Nishati Safi

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kampuni ya Hanspaul Group imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini wawekezaji wa ndani na Sekta binafsi kwani inawawekea mazingira rafiki na wezeshi ya kufanya shughuli zao.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Satbir Singh Hanspaul katika Ufunguzi wa Onyesho la Nane la Kimataifa ya Utalii (S!TE EXPRO 2024) yanayofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 
Amesema kuwa Serikali imeonyesha nia ya dhati ya kuthamini sekta binafsi kwani imetengeneza mazingira rafiki yanayowafanya wafanye shughuli za uzalishaji kwa tija.

" Naishukuru Serikali kwa jinsi inavyothamini sekta binafsi imeweka mazingira rafiki na wawekezaji wa ndani kwa kufanya hivi wawekezaji wataendelea kuongezeka," amesema Hanspaul.

Amebainisha kuwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi, kampuni hiyo imeleta magari yanayotumia nishati ya umeme katika sekta ya utalii.

Amesisitiza kuwa Serikali  imeweka na kuandaa Mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi jambo lililosaidia kampuni hiyo kutengeneza teknolojia mpya ya matumizi ya nishati ya Umeme katika magari ya Utalii, kwa lengo la kuwezesha kuwa na Utalii wa kijani.

Pia amesema kampuni hiyo itaendelea kuunga juhudi za Serikali za kutumia nishati safi kwani matumizi ya nishati hiyo yanasaidia kutunza mazigira huku akiongeza nishati safi inaipunguzia jamii kupata madhara yatokanayo na matumizi ya nishati zisizo salama.

Amefafanua kuwa magari yanayotumia nishati hiyo yataleta mapinduzi na kuchagiza watu kuanza kuyatumia kwani yana unafuu katika matumizi hususani kuwapunguzia gharama watumiaji.  



No comments:

Post a Comment

Pages